Habari za Punde

RAIS KIKWETE MGENI RASMI KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA CHUO CHA KIISLAMU CHA AL- HARAMAIN

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika harambee ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mufti wa Tanzania Sheikh Issa bin Shaaban Simba,  KATIBU Mkuu wa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleman Lolila (wa pili kulia), Kadhi Mkuu Sheikh Abdallah Mnyasi (kulia) na Shehe wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Alhad (kushoto) wakiomba dua baada ya harambee kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye hafla  iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiaga baada ya kuwa mgeni rasmi katika harambee ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi ambaye alichangia shilingi milioni 100 na Mwenykiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James  Mbatia aliyechangia shilingi milioni mbili  kwa ajili ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye harambee iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam (Picha na Ikulu )

1 comment:

  1. Wakristo wakichanga maendeleo ya kiislamu inaonekana ni sawa tu lkn. waislamu wakifanya hivyo kwa wakristo inakua nia ukafiri!

    Haya, mengi katoa milioni 100 kuchangia chuo cha kiislamu, tuone sasa UWAMSHO watatoa kiasi ngani?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.