Kikosi Kabambe cha Timu ya Wahifadhi Pesa Zanzibar Benki wa Watu wa Zanzibar, kilichoitowa jasho timu ya ZANTEL, na kuwaonesha wao sio watunza pesa na michezo wao nambari moja.
Kikosi cha timu ya Kampuni ya Simu ya Mkononi ZANTEL, kilichoilazimisha timu ya PBZ kutoka nao sare ya 2--2, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan.
Mshambuliaji wa timu ya PBZ Ashraf Abdalla kushoto na beki wa timu ZANTEL, Mohammed Mosmati wakiwania mpira wakati timu hizo zilipokutana katika mchezo wa kirafiki kupimana kiwango cha mchezo huo, na kuoneshana Kazi ndani ya soka.
Beki wa timu ya PBZ Ussi Nahoda , akijaribu kumzuiya mshambuliahi wa timu ya ZANTEL Hemeid Seif ,mwenye mpira akimtoka beki wa timu ya PBZ, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan.
Mshambuliaji wa timu ya Benki ya Watu wa Zanzibar Hassan Mwadini akimpita beki wa timu ya ZANTEL Haji Miraj , wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Amaan timu hizo zimetoka sare ya 2--2.
hawa pbz washawahi kushinda lkn kila siku wanafungwa tu
ReplyDelete