Habari za Punde

Vijana wa Jimbo la Kikwajuni Wapata Mafunzo ya Kazi Nje nje.

 Mkufunzi wa Mafunzo ya Kuwawezesha Vijana kupata Kazi, yalioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, kupitia Taasisi ya TAYI, yaliofanyika katika jengo la Maendeleo ya Uvuvi  Muembemadema Zanzibar kiliko Kituo hicho kilichoanzishwa na Mhe. Hamadi Yussuf Masauni katika jengo hilo na kutowa mafunzo mbalimbali kwa Vijana kujiandaa kupata Kazi na kujiendeleza na Biashara baada ya kupata mafunzo hayo.  
 Vijana wakishiriki katika mafunzo ya Kupata Kazi Nje nje, yanayofanyika katika Kituo cha Maendeleo ya Vijana wa Jimbo la Kikwajuni, kilichoanzishwa na Mbuge wao. 

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Hamad Yussuf Masauni, aliyesimama nyuma , akiwa na Wakufunzi wa  Mafunzo ya Kazi Njenje yanayofanyika katika Kituo cha Vijana cha Kuwaendeleza Kielimu wa Jimbo la Kikwajuni , alipotembelea mafunzo hayo yanayoendelea katika kituo hicho kwa Vijana wa Kwanza walioaza mafunzo hayo ili kujiajiri na kuajiriwa baada ya kupata elimu hiyo inayotolea na Taasisi ya TAYI.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.