Habari za Punde

Timu ya PBZ ikiwa katika Mechi za Kujipima Nguvu kwa Ajili Ligi ya Mabenki Zanzibar.

Kikosi cha Timu ya Wafanyabiashara iliotowa Onyo kwa Timu ya Benki ya Watu wa Zanzibar ambayo inajiandaa na Michuano ya Ligi ya Mabenki Zanzibar, yana yotarajiwa kuaza katikati ya mwezi wa Juni katika Uwanja wa Mao, na kushirikisha zote za Mabenki yalioko Zanzibar na kuishirikisha timu ya Wizara ya Fedha Zanzibar.Ligi hiyo imedhaminiwa kwa pamoja na mabenki ya KCB na PBZ, ili kutowa burudani kwa Wananchi na Wateja wa mabenki hayo na kutowa burudani kwa wapenzi wa mchezo wa mpira Zanzibar.Kikosi cha PBZ kinajinowa na michezo ya kirafiki ili kuweza kutowa Kombe hilo kwa mara ya kwanza kuazisha hapa Zanzibar kwa timu za Mabenki.
Beki wa timu ya PBZ Issa Mohammed, akijaribu kumzuiya mshambuliaji wa timu ya Wafanyabiashara  Salum Masoud, wakati wa mchezo wao wa kirafiki, uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya Wafanyabiashara imeshinda kwa mabao 5-1
Mshambuliaji wa timu yaWafanyabiashara Ali Said, akiwapita mabeki wa timu ya PBZ, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Amaan.kulia beki wa timu ya PBZ Ussi Nahoda, akijaribu kumzuia.
Wachezaji wa timu ya PBZ na Wafanyabiashara wakiwania mpira.
Mchezaji wa timu ya Wafanyabiashara Zanzibar Hamad Haji, akijiandaa kumpita beki wa timu ya PBZ Ussi Nahoda, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya Wafanyabiashara Zanzibar imeshinda.


Kocha wa Timu ya PBZ Ali Mwalim, akitowa maelekezo kwa timu yake wakati wa mapunziko ili kuweza kujirekebisha na kuweza kutowa mna ushinda lakini bahati haikuwa kwao na kuwezeshwa kupata kipigo cha mabao 5-1
Kiongozi wa timu ya PBZ akiwapa maelekezo jinsi ya kuweza kusawazisha mabao waliofungwa na timu ya Wafanyabiashara Zanzibar.iliofanyika katika uwanja wa Amaan.
Kocha wa timu ya Wafanyabiashara Zanzibar akitowa maelekezo kwa wachezaji wake katika muda wa mapumziko wakati timu hiyo ikiwa mbele kwa mabao 3-1




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.