Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, anatarajiwa kesho kuwa mgeni rasmin katika uzinduzi wa Umeme mpya baada ya kutandikwa waya huo mpya kutoka Ras Kilomoni Dar-es-Salaam hadi Ras Fumba Zanzibar.
Uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vya mpira Amaan kuanzia saa 2.30 asubuhi na kuhudhuriwa na wananchi na wageni mbalimbali .
Mradi huo mkubwa wa kutandika waya mpya wa umeme ulianza mwaka jana na kukamilika kwake mwaka huu mwanzoni mwa mwezi wa pili na kuwa katika majaribu kwa matumizi ya kawaida kwa wananchi wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment