Habari za Punde

Uzinduzi wa Maonesho ya Mei Mosi Amaan.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Mei Mosi katika viwanja vya Amaan.
Kaimu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Haji Omar Kheri, akihutubia katika ufunguzi wa maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Amaani

Ofisa wa TUICO akisoma hutuba ya Wafanyakazi katika uzinduzi wa maonesho ya Mei Mosi yanayofanyika katika viwanja vya Amaan.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar akikata utepe kuashiria kufunguwa Maonesho ya Wafanyakazi ya Mei Mosi katika viwanja vya Amaan,
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimsikiliza Afisa wa TIENS Salum Issa Baruan, akielezea matumia ya dawa za TIENS, alipotembelea banda lao wakati wa maonesho ya Mei Mosi katika viwanja vya amaan.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia bidhaa za Shirika la Biashara la Taifa ZSTC, zitokanazo na bidhaa za Mafuta ya Makonyo ya Karafuu na Mikaratusi na Michaichai, kutoka kwa Afisa wa ZSTC Silima Bakari.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Taifa Zanzibar ZSSF, Raya Hamad, akitowa maelezo ya huduma zinazopatikana kwa Wanachama wa Mfuko huo na faida yake kwa Wananchi wakati wa maonesho ya Mei Mosi yanayofanyika katika viwanja vya amaan.
Afisa Masoko wa Shirika la Posta Kanda ya Zanzibar Suwed akitowa maelezo ya huduma yao wanayotowa kwa Wananchi katika maonesho ya Mei Mosi na kutowa maelezo ya huduma mpya walizozianzisha hivi karibuni jinsi zinavyotowa fursa kwa wananchi kupunguza usumbufu kwa wateja wake wakati wa maonesho ya mei mosi.
Mfanyakazi wa Idara ya Mifugo akitowa maelezo ya ufugaji wa Kuku wa Nyama na Mayai katika maonesho ya Mei Mosi
Wanafunzi wa Kituo cha  Amali Mkokotoni, wakionesha jinsi ya mafunzo  ya amali wanayopata katika  wa  katika kituo hicho wakati wa maonesho hayo.
Mjasiriamali wa Bidhaa za Mwani Khamis Yussuf Machano (Babu hicha ) akitowa maelezo ya idhaa zao zitokanazo na mwani wa pwani kwa kutengeneza Jam, Keki na Vileja kwa kutumia mwani, kwa wananchi waliotembelea banda lao la Kikundi cha Ulezi Una Kazi Fujoni Unguja.
Wafanyakazi wa Kampuni ya soda ya COCA COLA wakionesha bidhaa yao ya iana ya Soda ya ZERO, katika maonesho hayo wakiwa katika banda lao wakisubiri uzinduzi wa maonesho hayo ya mei mosi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.


Mjasiriamali wa

  







1 comment:

  1. Kwa wenye kupenda coca cola tuwe pole angalia hii

    http://metro.co.uk/2012/06/27/coca-cola-and-pepsi-contain-traces-of-alcohol-482866/

    na hao wanaosema grand malt haina kilevi watajitetea vipi ikiwa coca cola ina kilevi , jee hii ambayo ina kila harufu na ladha ya pombe kuambiwa haina kilevi inaingia akilini? Nimefikisha ujumbe msije kusema hakuwa na taarifa.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.