Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Mkoa Mjini Magharibi Bwana Mohd Omar Said { Maarufu Kidevu } akielezea mkasa uliompata wa kumwagiwa Tindi kali { Acid } mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kumfariji.
Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Bwana Mohd Omar Said { Maarufu Kidevu } anaendelea kupatiwa huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa Tindi kali { Acid } na mtu asiyejuilikana.
Mkasa huo umempata jana usiku mara baada ya kurejea ibada ya sala ya Isha wakati akiendelea na harakati za kutafuta huduma za maji na kumwagiwa tindi kali hiyo iliyoathiri eneo la kifua chake, Bega pamoja na sehemu za jicho la kulia.
Hili ni tukio la tatu kutokea ndani ya mkoa wa mjini Magharibi likiwahusisha aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Ndugu Rashid Ali Juma pamoja na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga.
Sheha huyo wa Tomondo Bwana Mohd Omar Kidevu akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Hospitali hapo kumfariji pamoja na kumpa pole alisema alijikuta akimwagiwa tindi kali majira ya saa 2.00 za usiku na mtu asiyemfahamu.
Bwana Mohd Kidevu alisema Mtu huyo alianza kutimua mbio baada ya kufanikiwa kufanya dhambi hiyo kitendo ambacho akalazimika kuomba msaada kwa wasamaria wema lakini hatimae ilishindikana kutokana na kuzidiwa kwa maumivu makali yenye kuchoma kama moto.
Sheha huyo wa Shehia ya Tomondo aliendelea kumfahamisha Balozi Seif kwamba hali yake hivi sasa inaendelea vyema na ameshaanza kupata matumaini kufuatia jicho lake kuanza kuona ingawa bado anakabiliwa na maumivu katika sehemu yake ya usoni.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alimuomba Sheha huyo wa Tomondo kuwa na moyo wa subra wakati wa kipindi hichi kigumu cha huduma za matibabu.
Balozi Seif alimuhakikishia Bwana Mohd Kidevu kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kufuatilia ushauri utakaotolewa na Madaktari kuhusu tiba ya afya yake na kutoa msaada wowote utakaohitajika ili kuendeleza nguvu za huduma ya tiba yake.
“ Tutafuatilia ushauri watakaotupa Madaktari kuhusu afya yao. Na kama kuna wazo la kukusafirisha iwe Hospitali ya Rufaa Muhimbili au Nje ya Nchi basi sisi kama Serikali tuko tayari kulitekeleza hilo “. Balozi Seif alimuhakikishia Sheha Mohd Kidevu.
Akizungumza na vyombo vya Habari nje ya Wodi ya Mapinduzi Kongwe katika Hospitali Kuu ya Mmnazi Mmoja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali Kuu imesikitishwa na vitendo hivi viovu vinavyoleta athari kwa Binaadamu.
Balozi Seif alisema tabia hii mbaya inayoonekana kuanza kuchipua hapa Nchini ikibeba ufinyu wa imani inaanza kuleta hofu miongoni mwa wananchi katika kuendelea na harakati zao za kimaisha za kila siku.
Alisema Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itaendelea na uchunguzi wa kufuatilia matukio hayo na haitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwafikisha katika mkondo wa sheria.
Mungu mkubwa sasa alive mwatima tindikali kafaidika na nini? Aliyemwagia Hana to faulk na nguruwe hivi kufanya hivyo cuf kutakusaidieni nini? Ipo siku enough is enough na nyinyi munafurahia mzalendo haitakusaidieni, polish mupo wapi kwa hii bora polish iondoke ktk mambo ya Muungano ili vipewe nafasi vikosi vya SMz
ReplyDeleteNani aliesema kuwa waliofanya hivi ni CUF? Hiki ni kitendo kibaya kufanyiwa mtu yoyote. CUF hawawezi kufanya kitendo kibaya kama hiki. Hawa ni watu wasioitakia mema Zanzibar na wanatamani turudi kule tunakotoka katika uhasama wa kisiasa. Sijui kamakuna CUF ambae anapinga maridhiano ya kisiasa yaliyopo. Nafikiri tuwaachie polisi na sio "polish" wafanye kazi yao ili wajue waliohusika na tukio hili.
DeleteNa serikali nayo inachangia kuendelea uharamia huu. Ikiwa serikali inajali raia wake basi ipo haja kuitungia sharia ya kuifanya ''acid'' itambulike ni silaha ya maangamizi na ni kosa la jinai raia akikutwa nayo. Iwe serikali inatoa kibali kwa muingizaji na msambazaji. Raia akiitaka kununua nilazima atoe Identity Card yake ya uraia na contact numbers za simu zake ili pindi likitokea kosa la jinai basi serikali ianze kwa muingizaji na msambazaji ili apatikane alie mtendaji. Haya yote yanawezekana .Get well soon ndugu shekha
ReplyDeleteB Khatib
Mtoa maoni wa kwanza,
ReplyDeleteHapana shaka hiki ni kitendo kiovu kufanyiwa binadamu yoyote, dhulma haikubaliki kwa yoyote awe wa chama chochote. Ulipokosea ni kulielekeza kosa hilo kwa CUF - unapandikiza chuki ambazo wewe mwenyewe humjui nani kafanya, ni dhana.
Pili ni kukerwa kwako na mzalendo, mzalendo ni chombo cha Wazanzibari wenye uchungu na nchi yao na kama kinakukera mbona utapata maradhi ya kujitakia!, tegemea muendelezo zaidi wa ukosoaji/kusiku kutoka mzalendo.net - kasi haitopunguzwa.
Kwa nguvu zote za hoja tunapinga udhalilishaji wa binadamu wa aina yoyote.
Tusikatae, cf ,muamsho wana furahia mambo hayo sasa nani? kama siwao ndio wanao lalamika hawapewi vitambulisho au vipande vya kura sasa kilukatili utako fanya wao hufurahi, hakumbuki kusisi tulitenga na jamii yetu kwa kuwaunga mkono wao na tulikuwa na hasira pale walipo onewa .Sasa hawajapata mombo ndohayo wakipa siwatakunya barabarani ikiwa mnafurahia tindikali je?tukiuliwa?
ReplyDeletePole zake sana sheha kidevu, lakini hili ni onyo kwa wale wote wanaofanya uhuni katika uongozi.
ReplyDeleteNaanza kupata picha ya kule tunakoeleke, mtu akifanya uhuni ajue zanzibar ya jana sio ya leo.
Wewe Ukimuona Mru anaanza Kuwavumishia watu au kikundi Fulani Uongo ujue hao ndio Wahalifu wenyewe...
ReplyDeleteNinani asiejua kama CCM UVC wakisaidiwa na Watanganyika ndio Wanaotaka kuisubortage Amani na Usalama wa Zanzibar na Wazanzibari?...
Tena kwasababu Wazanzibari wanataka Muungano wa Mkataba.. Hivyo Limbukeni CCM na Maharamia Wanaowaleta kupitia Makanisa ndio wanofanya vitendo vyote vya Kijahili Zanzibar ..Halafu ndio hao wanakuja kwenye Mtandao kama huyu BUNJU alietoa Maoni juu ya CUF na Muamsho...
Wewe Kibaraka wa Tanganyika Nenda Shule ukasome alama za Nyakati na acha kuilaumu CUF... Nyinyi ndio wenye Silaha na hamutaki Wazanzibari waseme ukweli... Washenzi nyinyi... ooooh CUF...Uamsho...Upemba... Mumefanya mengi machafu nyinyi Washenzi Wakubwa...
Kazi zenu kutaka madaraka hata kama hamuna wezo wakuongoza Nchi...Siajabu hata Hao asheha wawajui hata kusoma na Kuandika munawapatia Usheha kwasababu inawalinda... Kila kiongozi wa CCM amevimba Tumbo kama Ana mimba ya watoto kumi...
Mumakaa madarakani kwa muda wa mika 50 sasa tunachokiona ni kuizamisha Zanzibar nakuwafanya Watoto wa Kizanzibari Wajinga... Ssa munaanza kuwabugudhi hata wale CCM ambao wanataka mabadiliko... Wacheni kuvumisha rumar mulizokua hamuna uhakika nazo..
Uwo nkaba hauji ng"o sisi tulitaka serekali3 hao wanojifanya cuf leo ndio walojipendeza kwa bwanawao rais wetu, Mh jumbe akafukuzwa uraisi wao wakapewa kilemba cha ukoka baada ya kusaliti nawao waksalitwa, sasa wasijifanye wanauchungu kumbe wao wenye mahasidi wa Zanzibar
ReplyDelete