Habari za Punde

Dk Shein amtembelea Sheha wa Tomondo

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuangalia Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja,Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) jinsi alivyoathirika na Tindikali alilomwagiwa na Mtu asiyejuilikanwa huko Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake,Sheha huyo yupo katika Hospitali ya Mnazi mmoja kwa matibabu,wa kushoto Dk.Slim Mohamed Mgeni,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja,Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) aliyetiwa Tindikali na Mtu asiyejuilikanwa huko Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake,Sheha huyo yupo katika Hospitali ya Mnazi mmoja kwa matibabu,wa pili kulia Kaka yake Sheha Sudu Mgeni Saidi
 
Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

1 comment:

  1. Huu ni Ujahili mkubwa wakuwamwagia Watu Tindi kali.. Lakini kwa vile Masheha wapo kwa ajili yakuwasaidia CCM kukaa Madarakani kimabavu na kuwanyima Wazanzibari ZID na Mambo mengine... Watu wameamua kuchukua hatua Mikononi mwao...

    Mimi nailaumu Serikali ya Dr Ali Mohamedi Sheni Inafuata Ilani ile ile ya CCM-Wabague Wazanzibari ili Waendelee Kutawaliwa na Tanganyika...

    Ndio Maana Watu hawana imani na Masheha hao.. Ujuzi wao wa Elimu ni Mdogo na hakuna asiejua kama Masheha ndio Kimbilio la Warioba na Mchakato wa Katiba..

    Kuna kesi nyingi ambazo zimetokea juu ya Masheha kuwanyima watu Barua za kupata haki zao au Kuwakanusdha Wazanzibari kwamba wao sio Wazanzibari... Hata hivyo hastahiki kumwagiwa tindi kali.. lakini ni mafunzo kwa masheha wengine.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.