Habari za Punde

Maalim Seif: Nitaomba kuwania tena urais mwaka 2015

Dar es Salaam. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema ataomba tena kugombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
 
Akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV, Maalim Seif alisema kuwa anachoomba tu Mwenyezi Mungu ampe afya njema.
 
“Ni uamuzi wa wananchi na wanachama wenyewe wa CUF lakini kama Mwenyezi Mungu akinipa afya na uzima bado nia ipo,” alisema Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
 
Alisema hivi sasa chama hicho kimekuwa kikijiimarisha visiwani huko kwa kufanya mikutano Pemba na Unguja ili kuhakikisha kinaendelea kukubalika kwa wananchi.

Kauli hiyo ya Maalim Seif ambaye amekuwa akiwania nafasi hiyo tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi, ilipokewa kwa hisia tofauti ambapo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bashiru Ali alisema vyama vya siasa ni lazima viwe vinatayarisha viongozi wa baadaye ambao watafahamu kwamba uongozi ni dhamana wanayopewa na wananchi.
 
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema Maalim Seif kama mwanachama wa chama hicho anaruhusiwa kwa mujibu wa Katiba kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa dola.

Chanzo - Mwananchi

5 comments:

  1. Jamani huyu mzee anapenda demokrasia kweli? tokea 1995 mpaka leo na bado anatarajia kugombea tena 2015!

    Hivi katika CUF bado hakuna anaeweza kugombea badala yake au ndio huo ubinafsi wenyewe huo?

    Ama kweli "Beautiful ones are not yet born"

    ReplyDelete
  2. GOMBANIYA WEWE BASI HUJAKATAZWAAA

    ReplyDelete
  3. A/a kwa ufahamu wangu Mdogo Makamo wa rais Zanzibar kasema kuwa Atagombea Uraisi 2015!! Hakusema hakuna ruhusa watu wengine wasigombee!! Kama kuna mtu anahisi hafaii basi it's your choice not to vote him!! No one is forced to vote for him!!! Tunasubiri kificho na yeye asema atagombani uwakilishi and then kuwa spika wa baraza still it's his decision!!! Hiyo ndio demokrasia

    ReplyDelete
  4. Anonymous wa tatu, nakubali maneno yako huyu MAALIM hana tofauti YOYOTE na akina KIFICHO!

    Lakini UWAMSHO na baadhi ya wana CUF waliwahi kusema mara nyingi tu kwamba maalim hana tofauti na wana CCM wengine.

    Aliulisha watu, akawafukuzisha kazi na wengine kuwachezesha "melody" kumbe shida yake ilikua ni madaraka tu, sasa sijui yeye na rafki yake KIFICHO watastaafu lini!

    ReplyDelete
  5. Huyuyu jamaazake hawamjui maalim ni kibaraka wasiku nyingi anawazuga,mabanchicha wenziwe

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.