Habari za Punde

Mradi wa kuwapatia chakula cha mchana wanafunzi wa skuli ya kusini



 


 
 
Mradi wa kuwapatia wanafunzi wa Skuli ya Kusini iliyopo Makunduchi waanza rasmi kwa majaribio jana. Akizinduwa rasmi mradi huo mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kusini, ndugu Faida Khamis Ali (wa tatu kutoka kushoto) aliwataka uongozi wa Skuli ya Kusini kuuenzi mradi huo kwa kutumia fedha za wafadhili kama zilivyokusudiwa.
 
Wakati huo huo mratibu wa mradi huo ndugu Mohamed Muombwa ambaye pia ni msaidizi wa Makamo wa pili wa rais, amesema mradi huo unaofadhiliwa na skuli rafiki Sundsvalls Gymnasium kutoka Sweden utawapatia chakula cha mchana wanafunzi wote 1000 kutoka msingi na sekondari.
 
Alisema kwa kuanzia chakula hicho kitatolewa wiki mara moja kwa kipindi cha mwezi mmoja. Malengo ya baadaye ni kuwapatia wanafunzi chakula cha mchana kwa siku zote 5.
 
Jumla ya shillingi 1.3 milioni zilitumika kugharamia mlo huo wa mchana. Kati ya fedha hizo shillingi 600,000 zilitumika kununua ng'ombe kwa ajili ya kitoweo.

2 comments:

  1. Hongera sana na sana Muombwa keep it up haya ndo mambo yanayotakiwa kufanywa km mzanzibar unatakiwa kujiuliza utaifanyia nini nchi yako na si kuwatia wenzako tindikali

    ReplyDelete
  2. Mradi Mzuri lakini kwanini Wapikiwe Pilau na Zijazwe Sahani tele.. Wakeshakula si Watataka kitanda cha kulala?...

    Naona Chakula kingi...Mradi wakuwaptia Wanafunz mlo ni mzurio lakini naona wangepatiwa Chakula ambacho kitajenga Mwili kama vile Combination ya Fibri foods, snaks, frugt salad & variaty of vegitables... Hivyo ndivyo vyakula wanavotakiwa wapatiwe .

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.