Tume ya Uchaguzi Zanzibar, (ZEC) imewataka
Wadau wa Uchaguzi katika Wadi ya Ng’ombeni Mkoani Pemba, kuipa mashirikiano
Tume hiyo , ili iweze kufanya Uchaguzi
mdogo wa Wadi hiyo kwa misingi ya Amani
na Utulivu na Wasivipe nafasi Vyama
vyao kupata kuwagawa kwa misingi
hiyo.
Akizungumza na Wadau wa Uchaguzi wa Wadi ya Ng’ombeni ,
Mwenyekiti ZEC, Zanzibar, Salmin Senga
Salmin, huko Mkoani ,wakati alipokuwa akifunguwa Semina ya Wadau wa Uchaguzi wa
Wadi hiyo ambao iliwashirikisha Wadau mbali mbali wakiwemo Wawakilishi wa Vyama
, NGOs, watu wa Serikali na nk.
Alisema
kuwa Wadau ni muhimu katika kuendesha
Shughuli za Uchaguzi kwa vile wao ndio
Wapiga kura katika maeneo yao
ambapo bila ya wao hauwezi kufanyika.
Mwenyekiti huyo aliwataka Wadau hao
kuhakikisha kuwa Jazba za Kisiasa hazipewi nafasi katika Uchaguzi huo kwa
kukumbuka kuwa wanaogombea wote ni watu wamoja na tafauti yao ni kwa Vyama lakini Umoja ni kitu muhimu.
Alifahamisha kuwa Utafanyika kwa mujibu wa
Sheria za Uchaguzi zilizopo nchini, ambazo zilitumika katika Uchaguzi mkuu
uliopita ambazo zimetungwa na Baraza la Wawakilishi.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa Wapiga kura
ambao wataruhusiwa kupiga kura hiyo ni wale tu ambao majina yao yamo katika
Daftari la Kudumu la Wapiga kura, ambalo lilitumika katika Uchaguzi mkuu na sio
vyenginevyo na kutumia Vitambulisho vyao vya Mzanzibar Mkaazi kama hapo awali.
Uchaguzi wa Wadi hiyo utafanyika kufuatia
tarehe 23 /6 mwaka huu , kufuatia kifo cha cha aliekuwa Diwani wa Wadi hiyo,
Massoud Khamis Omar , ambae alifariki tarehe 26/5/2012, ambapo Tume ya Uchaguzi
imeshajiandaa.
Akitowa mada katika Semina hiyo, Msimamizi
wa Uchaguzi Wilaya ya Mkoani, Seif Salim
Juma, alisema kuwa Uchaguzi mdogo wa Wadi hiyo utafanyika kwa mujibu Sheria ya
Uchaguzi Namba 11 ya Mwaka 1984 kifungu cha 45(1) (b) .
Alifahamisha kuwa katika kufanikisha Uchaguzi
huo Tume itatumia Daftari la kudumu la Wapiga kura lililotumika kwa Uchaguzi
mkuu mwaka 2010 na kwa maana hiyo
hakutokuwa na kazi ya Uandikishaji wapiga kura kwa Uchaguzi huo na inakadiriwa
kuwa Wapiga kura 1,297.wataendesha zoezi hilo.
Seif, alieleza kuwa Tume ya Uchaguzi
itaweka hadharani Daftari la Wapiga kura walioandikishwa katika Wadi hiyo siku ya tarehe 15/5 /2013 ,
siku saba kabla ya siku ya Upigaji kura na kura zitapigwa katika Vituo ambavyo
vilitumika katika Uchaguzi uliopita 2010 ambayo ni Skuli ya Maandalizi Ng’ombeni .
Nae, Khamis
Issa Khamis, Mkuu wa Divisheni ya Sheria
Tume ya Uchaguzi Zanzibar, akitowa mada kwa Wadau wa Uchaguzi wa Wadi
hiyo alieleza kuwa kuwa Uchaguzi huo wa Wadi ya Ng’ombeni, utaratibiwa na
kuendeshwa na Tume kwa mujibu wa Sheraia
za Uchaguzi zilizopo kwa lengo la kuweka utaratibu mzuri na wazi wa kuwapata
Viongozi wa Wananchi katika njia ya Kidemokrasia .
Alifahamisha kuwa Sheria hiyo imetumika
tokea Uchaguzi wa Chama kimoja 1985 na 1990 na baadae kufanyiwa marekebisho
makubwa ili iendane na mfumo wa Vyama
vingi vya Siasa ulioanzishwa mwaka 1992.
Hata hivyo, alisema kuwa mambo ambayo
yamekatazwa katika Chaguzi zilizofanyika pia zitatumika katika Uchaguzi huo na
wala hakuna mabadiliko mengineyo.
Aidha , Afisa Habari na Mahusiano wa ZEC,
Idrisa Haji Jecha, akitowa Mada kwa Wadau hao alisema kuwa Kisheria kazi ya
kuendesha Uchaguzi mdogo wa Wadi ya Ng’ombeni ni ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar , lakini Tume
pekee haiwezi kufanya Uchaguzi bila ya kuwashirikisha Wadau.
Alisema kuwa Wadau wa Uchaguzi wanao
umuhimu wa kipekee kwa vile kuosekna kwao katika mchakato wa Uchaguzi hupelekea
Uchaguzi husika kuharibika na kuwepo kwao kunapelekea ufanisi katika Uchaguzi
huo.
Jecha ,alisema kuwa ZEC, inahistoria ndefu
ya kuwashirikisha Wadau wa Uchaguzi katika harakati mbali mbali za Kiuchaguzi ,
na inafanya hivyo kwa vile inaamini kuwa Wadau ni watu muhimu katika kuendesha
Shughuli za Uchaguzi .
Alifahamisha kwa kuwa Tume inatambuwa umuhimu wa Wadau
ili kufanikisha Uchaguzi huo inawaomba Wadau hao , kufanikisha Uchaguzi huo,
kwa kuhakikisha kuwa unafanyika kwa Amani na Utulivu, kusaidia Wananchi
kuheshimu na kufuata Sheria za nchi na za Uchaguzi sambamba na kuwaelimisha
Wananchi kutokiuka Sheria na maadili ya Ucahguzi nk.
Akifunga Semina hiyo Mjumbe wa Tume ya
Uchaguzi ZEC, Ayoub Bakar Hamad, aliwataka Wadau hao kuwa na Uvumilivu wa
kisiasa kwani kila siku zinapokwenda hali imekuwa mzuri kisiasa jambo ambalo
halikutegemewa kama lingetokea.
No comments:
Post a Comment