Habari za Punde

Hafla ya Kutimia miaka 93 Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Aboud Jumbe Mwinyi Nyumbani Kwake Migombani Zanzibar.

Sheikh. Zuber Yahya akitowa maelezo ya shughuli ya Dua kwa kushrani kuwaombea Ndugu na Jamaa wa Mzee Alhajj Aboud Jumbe wakati wa hafla ya kutimia miaka 93 ya kuzaliwa kwake iliofanyika katika viwanja vya Nyumbani kwake Migombani mjini Zanzibar  
Ustadh Muhammad Hajji Yoyota akisoma risala ya maombi, matumaini na shukrani kutoka kwa Mzee mwenyewe Alhajj Aboud Jumbe, wakati wa hafla hiyo akiosoma kwa niaba ya Mzee Jumbe.
 kwa kutimiza miaka 93 ya kuzaliwa iliofanyika katika viwanja vya nyumbani kwake migombani na kuhudhuriwa na ndugu na jamaa na Wajukuu wa Mzee Jumbe.

Waalikwa waliohudhuria hafla ya shukrani ya kutimiza miaka 93 kwa Mzee Jumbe iliofanyika katika viwanja vya nyumbani kwake migombani Zanzibar.

Mtoto wa Mzee Jumbe Mustafa Aboud Jumbe akitowa shukrani kwa niaba ya Familia ya Mzee Jumbe kwa Wananchi waliohudhuria hafla hiyo kuungana na familia yao kumuombea Mzee Jumbe katika hafla yake ya kutimia miaka 93 ya kuzaliwa.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Ahajj Khamis Haji Khamis akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliofanyika nyumbani kwake  Mzee Jumbe Migombani Zanzibar. 

Wajukuu wa Mzee Jumbe wakihudhuria hafla hiyo ya Babu yao kutimiza miaka 93 ya kuzaliwa kwake.

3 comments:

  1. Allah kumpa uhai azidi kutubia makosa yake..na kwa kweli huyu mzee umri wake anautumia vizuri.

    Naamini siku akiingia kaburini, ataona bora vile alivyolazimishwa kujiuzulu ili aepukane na fitna na siasa.

    ReplyDelete
  2. Yeye anajuwa hivyo ndio maana hata zile zilizokuwa Birthday za Nyerere alikuwa haendi kutokana na kufuru za mchonga!!! Mchonga kufuru yake ya mwisho alisema ataishi kama alivyo ishi mama ake labda agongwe na Basi!! Hapo kufuru zilizidi ikabidi ALLAH amuondoe bila kugongwa na basi!! Maana kibri hakifai na binadamu huna guarantee!! Utaishi miaka mingapi!! Hiyo ni siri yake mwenyewe ALLAH na wala hujui Nchi gani atakufa.

    ReplyDelete
  3. Huyu mzee alikuwa hendi si kuwa akilikuwa ana ogopa kufuru , alizokuwa anafanya Nyerere, bali ni bifu lake lamoyoni, Nerere, simuislam, kwahiyo aliyo kuwa anafanya ni sahihi kwa dini yake, kukufuru hukufuru wale walio amini na waka mcha mungu, likini mtus si muislam, ukisema alikuwa ana kufuru sijui tukuelewe vipi?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.