Na Waandishi wetu
HATIMAYE bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, imepita baada ya kufanyiwa marekebisho.
Bajeti hiyo ilirejeshwa juzi ili kutoa nafasi kwa wizara na kamati ya viongozi wa kitaifa ya Baraza la Wawakilishi, kuipitia upya.
Wawakilishi walikubali kuipitisha bajeti hiyo baada ya Waziri, Fatma Abdulhabib Fereji kufafanua jinsi fungu la Tume ya Ukimwi ambalo ndio lililozua mjadala, lilivyofanyiwa masahihisho.
Mapema Mwenyekiti wa Kamati , Hamza Hassan Juma, alisema kamati yao kwa kiasi kikubwa imeridhika na masahihisho yaliofanywa.
Akitoa maelezo yake baada ya ufafanuzi huo Mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu alisema ,ingawa kumefanyika masahihisho katika fungu hilo, lakini kutahitajika uwepo umakini kwa kamati za baraza pale watapokuwa wanapitia matumizi ya wizara.
Alisema kinachoonekana katika matumizi ya serikali baadhi ya watendaji hupanga matumizi yenye utata, kwani hata baadhi ya hoja wakati walipokaa katika kamati hiyo kuna mambo yalionekana kutokuwa na majibu.
Mwakilishi huyo, alimpongeza waziri wa wizara hiyo kwa kukubali kufanya ufafanuzi juu ya hoja ambazo zilionekana kuwa na utata.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, alisema serikali inakubaliana na jitihada zilizochukuliwa na viongozi wa Baraza la Wawakilishi kwa dhamira ya kuimarisha utawala bora.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, aliipongeza hatua ya Mwakilishi huyo kutambua baadhi ya maeneo yenye utata.
Kuhusu fedha za vifaa zilizotengwa kwa ajili ya Pemba, alisema ni kweli fedha hizo ni nyingi kutokana na fisi zimechoka na hazina vifaa na kama kuna wasi wasi utaweza kuondolewa kwani.
Hata hivyo, Waziri huyo alimtaka Mwakilishi huyo kukubaliana na baadhi ya hoja kwa vile nia ya serikali ni kuhakikisha kuwanakuwa na matumizi bora ya serikali.
Aidha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, aliipongeza hatua ya Mwakilishi huyo kuweza kutambua baadhi ya maeneo ambayo yalionesha kuwa na wasi wasi nayo.
Mapema Spika, Pandu Ameir Kificho amezitaka Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi kufanya kazi kwa makini zinapopitia bajeti za wizara ili kuondoa kasoro zinazojitokeza.
Akizungumza wakati akiahirisha kikao cha baraza jana asubuhi, kufuatia juzi wawakilishi kukataa baadhi ya vifungu katika bajeti ya ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Spika Kificho alizitaka kamati hizo ziwe makini.
Alisema kutofanya kazi ipasavyo kwa kamati hizo ndiko kunakosababisha kukwamisha baadhi ya vifungu vya matumizi ya fedha wakati wa kujadiliwa.
Spika alisema kamati zina jukumu kubwa la kuhakikisha wanaichunguza bajeti pamoja na kuitoa kasoro zote ambazo zitajitokeza kabla ya kuwasilishwa barazani kujadiliwa.
“Kamati mnapoletewa hotuba ya bajeti mhakikishe kwamba mnaipitia kwa makini ili wajumbe wanapokuja kuipitisha kusiwe na kasoro,” alisema.
Aidha alisema waziri anaehusika lazima ahakikishe anatoa vizuri majibu ya masuala yote yanayoulizwa na wawakilishi.
“Mawaziri mnapokuja kuwasilisha hotuba za bajeti zenu mhakikishe mnajua kila kitu kilichomo ndani yake kwa kuwauliza wasaidizi wenu kama Makatibu na wengineo ili mnapoulizwa mtoe ufafanuzi sahihi,”alisema.
Alisema kuchelewa kupitishwa bajeti ya ofisi ya Makamu wa Kwanza kumeanza kuathiri muda wa kikao hicho na si busara kwa baraza la wawakilishi kutumia fedha zilizo nje ya matumizi. (habari hii imeandikwa na Mwantanga Ame, Kauthar Abdalla na Asya Hassan).
Labels
- .
- `
- 8
- AFYA
- AFYA.
- AJALI
- BIASHARA
- BURUDANI
- DINI
- ELIMU
- FILAMU
- HABARI
- HARUSI
- HOSPITALI
- I
- JAMII
- KATUNI
- Kii
- KILIMO
- KIMATAIFA
- KITAIFA
- Ku
- MAGAZETI
- Mahkamani
- MAISHA
- MAKALA
- MAKALA AFYA.
- MAKALA.
- MATUKIO
- MATUKIO.
- MICHEZO
- MITAANI
- MIUNDOMBINU
- MSAADA
- Ok
- SIASA
- TANGAZO
- TAWA YAWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI
- TEKNOLOJIA
- UCHUMI
- UTAFITI
- UTALII
- VIDEO
- VIJANA
- VISA INTERNATIONAL YAZINDUA TAWI TANZANIANa Mwandishi wetu 16.07.2025DAR ES SALAAM
- WEZI
Tafsiri ya Lugha
Popular Posts
-
Na Mwandishi Wetu, West Kilimanjaro Jamii imetakiwa kushirikiana kikamilifu katika kudhibiti uharibifu wa mazingira ili kupunguza athari za ...
-
Mshambuliaji wa Timu ya JKU akimpita beki wa Timu ya Muembemakumbi City wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar PBZ Priemer League mche...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar in...
-
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo...
-
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imefanya ziara kisiwani Pemba kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika Afisi za Tume ya...
-
Na Mwandishi Wetu, JAB Vitambulisho vipya vya kidijitali vinavyoendelea kutolewa na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) vimepokele...
Home
Hatimae bajeti Makamu wa Kwanza wa Rais yapita. Spika azitaka Kamati kuongeza umakini zinapopitia bajeti
Hatimae bajeti Makamu wa Kwanza wa Rais yapita. Spika azitaka Kamati kuongeza umakini zinapopitia bajeti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
BLOGU RAFIKI
-
-
RC KUNENGE: TUNATAKA PWANI YA KUTATUAMIGOGORO KWA UBUNIFU WA KIMKAKATI - Na Khadija Kalili , Pwani MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge, amesema serikali ya Mkoa imelenga kuifanya Pwani kuwa kinara wa ubunifu na utatuz...2 hours ago
-
Elimu : Bajeti za Elimu Zisipuuzwe wakati wa misukosuko ya Kiuchumi na Kisiasa Duniani - Kikwete na Malala Waonya. - Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Malala Yousafzai, wameonya juu ya mwenendo hatarishi duniani wa kupunguza au ku...14 hours ago
-
MAHOJIANO YA TAUSI SUEDI NA AMRI NGOYE KUHUSU CSI KUPITIA KWANZA PRODUCTION NCHINI MAREKANI - Pata habari motomoto kupitia facebook kwa kulike huu ukurasa wetu https://www.facebook.com/pages/Pamojapureblogspotcom/312633955485619?ref=hl7 years ago
Marafiki Duniani
Popular Posts
-
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili Zanzibar majira ya mchana kwa Ndege na kuendelea na taratibu za Maziko yatafanyika katika Mtaa wa...
-
The United Republic Of Tanzania National Examination Council of Tanzania Form Four Examination Results 2017/2018 The National E...
-
Makamanda wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Waziri Kiongozi wa Kwanza wa Zanzibar na Brigedia Jenerali Mstaaf Ramadhani Haji Faki...
-
Na Miza Kona/Rahma Khamis Maelezo-Zanzibar Jumla ya wanafunzi 16,744 wamechaguliwa kuendelea masomo ya kidatu cha tatu kati ya wanafun...
-
Bwana Harusi Lusajo Sajent Mwangambaku (kushoto), akiwa katika pozi na mke wake Neema Stanley Matowe katika hafla yake ya ndoa iliyofa...
-
Mama mjazito akihangaika na hatimaye kupoteza maisha kutokana na mimba za utotoni..Video ipo hapo chini baada ya maelezo mafupi
-
Hutuba ya Mhe Waziri wa Afya Nd. Mahmoud Thabit Kombo kwa Waandishi wa Habari Katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Dunia Zanzibar, 22...
-
Madawa na Maji vilivyokabidhiwa na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya Kambi za K...
Samahani sana Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Ili iris wa bila ya kufanyiwa
ReplyDeletecoyote . Ni muhimu kuweka taarifa kwa usahihi tujitahidi kupata taarifa kwa usahihi wake