Habari za Punde

Iran yaadhimisha kifo cha Imam Khomain

Na Kauthar Abdalla
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Said Ali Mbarouk amesema mafundisho ya Imam Khomain baada ya kuitawala Iran yameleta mabadiliko makubwa katika dini ya kiislamu.

Alisema Iran ilikuwa imepotea lakini Imamu huyo aliweza kuirejesha katika muongozo mzuri na mafundisho yameenea kutokana na jitihada zake za kuimarisha uislamu nchini humo kwa kufanya mapinduzi dhidi ya serikali iliyokuwa madarakani mwaka 1979.

Waziri Mbarouk alisema hayo alipokuwa katika hafla maalum iliyofanyika katika kituo cha utamaduni wa Iran Mlandege ya kumkumbuka Imam Khomain kwa kutimia miaka 24 tokea kufariki .

Kiongozi huyo alifanya mapinduzi makubwa ya kuikomboa dini ya kiislamu iliyokuwa ikipingwa na serikali iliyokuwa madarakani .

Aidha alisema Khomain alifika sehemu ambayo ulimwengu ulimuhitaji kutokana na hali ya mazingira ilivyokuwa Iran ilihitaji mapinduzi ya haraka hali ambayo ilipelekea kubadilisha maisha ya waislamu.

Aliwataka waislamu kumkumbuka Imam huyo kwa kufuata taaluma na mafundisho yake kwa vitendo.

Nae Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mendi Aghajafari alisema baada ya mapinduzi ya kiislamu Iran iliimarika na kusimama imara kiuchumi, kwani aliweza kuitoa nchi hiyo katika mikono ya ukoloni na unyonyaji licha ya vikwazo ilivyokuwa ikikumbana navyo.

Alisema baada ya mapinduzi hayo Iran ilipata maendeleo makubwa ya kisayansi katika mambo mbali mbali kutokana na taaluma aliyokuwa nayo Khomain pamoja na kutoa mashirikiano bila kujali tofauti za kidini.

Sambamba na hayo faida iliyopatikana katika Mapinduzi ya kiislamu ni kubwa katika Nyanja zote ni vyema yakaenziwa ili kuweka kumbukumbu nzuri kwa kizazi cha baadae ambapo ni miaka 34 sasa tokea kufanyika kwa mapinduzi hayo.

4 comments:

  1. Innalillahi wa Inna ilayhuraajiuun Nakupa pole Waziri kwa kukosea au kutokujuwa kuwa Mashia sio wa islamu.
    Tuwe na tahathari na iwapo ni kisiasa kwa Allah hakuma siasa siku ya hukumu,iwapo umepotosha utakuwa na dhimma kwa ulio wapotosha.

    ReplyDelete
  2. Sisi tunasema madam wametamka kalima ya 'Laa ilaha, illa llah, Muhammada rasulu llah' tunajua ni waislamu, mambo mengine tena anajua M/Mungu.

    Umma wa kiislamu, umechoshwa na kugawanywa kwa misingi ya madhheb na kuonewa na mataifa ya magharibi kwa kutumiwa watu kama nyinyi.

    Heri ya hao shia kuliko Sunni wa Saudia wanaoshirikiana na marekani kuuwa watu wasio hatia LIBYA, SYRIA, IRAQ n.k

    ALLAH AMSHAMEHE MAKOSA YAKE NA AMPUMZISHE KWA AMANI IMAMU KHOMEIN...AMINI!

    ReplyDelete
  3. Naam ni kweli mashia sio waislam mtoa maoni wa mwanzo upo sawa kabisa, mashia hawana laila haila llah yoyote! wanasema saydna ali ni bora kuliko mtume, wakiomba dua zao hutaja maimamu wao 12 dua lazima ipitie kwa imamu kwanza, hio ni shirki kubwa, ibada zao mashaka matupu ukiyajuwa utawakalia mbali.

    ReplyDelete
  4. Anojua dheb ilipini sahihi ni mungu mwenye,wewe unowita mashia, makeiri wewe usim wako ukawapi?.ungetutole aya inosema hivo, utashiwako na unachokipenda wewe,ndio uislam sasahi tupe vigezo vya huo ukafiri wa kishia,usimcheke kibogo kwa kuwa wewe unapengo

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.