Kikosi cha timu ya Uhamiaji kinachoshiriki Kombe la Mabenki kiliilazimisha Timu ya Benki ya Watu wa Zanzibar sare ya mabao 2--2, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Mao.
Mchezaji wa timu ya Uhamiaji Twahir Hassan mwenye mpira akimpita beki wa timu ya PBZ Said Khamis, katika mchezo wa Kombe la Mabenki Zanzibar. timu hizo zimetoka sare ya 2--2
Hekaheka katika goli la timu ya PBZ
Wachezaji wa timu yaUhamiaji na PBZ akiwania mpira
Benchi la wachezaji wa timu ya Uhamiaji wakiwa na majonzi baada timu yaokufungwa bao la pili na mchezaji wa timu ya PBZ Ali Mwimjuma.
Mchezaji wa timu ya PBZ Othman Mzee, akimiliki mpira na kumzuiya mshambuliaji wa timu ya Uhamiaji
Mchezaji wa timu ya Uhamiaji Said Ali akimpita beki wa timu ya PBZ Said Khamis.
Beki wa timu ya PBZ Mwalim Hassan, akimzuia mshambuliaji wa timu ya Uhamiaji Said Ali,katika michuano ya Kombe la Mabenki ya Zanzibar yanayyofanyika katika uwanja wa Mao.
No comments:
Post a Comment