Habari za Punde

Makamu wa Rais Dk. Bilal Atembelea Chuo Kipya cha Tehama cha Veta Kipawa Jijini Dar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza machache baada ya kutembelea na kujionea Teknolojia ya ufundishiaji inayotumiwa na walimu wa Chuo hicho cha VETA Kipawa.
 Sehemu ya wanafunzi, walimu wa Chuo hicho waliohudhuria, wakimsikiliza makamu wakati akizungumza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mwalimu wa Umeme katika Karakana ya mafunzo, Adrian Aloyce, wakati akifafanua jinsi Mashine za 'Automatic System' zinavyoweza kujiendesha zenyewe, wakati Makamu alipotembelea katika Chuo kipya cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam, leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza na kumtazama Mwanafunzi wa umeme, Elia Michael, alipokuwa akielezea jinsi wanafunzi hao wanavyoweza kuunda Sacket ya umeme inayoweza kuongoza mashine mbalimbali za umeme, wakati Makamu alipotembelea katika Chuo kipya cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam,
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Umeme Eunice Urio, wakati akimfafanulia kuhusu utendaji kazi wa Mashine ya kufundishia jinsi inavyoweza kuongoza mashine mbalimbali za umeme, wakati Makamu alipotembelea Chuo kipya cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam, leo



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.