Na Fatuma Kitima,DSM
JESHI la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limewatia mbaroni majambazi 22 wanatomia silaha kali za moto.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova alisema majambazi hayo yamekuwa yakiwalenga wageni, wawekezaji ambao wanasafirisha pesa zao bila kuchukua tahadhari.
Alisema majambazi hayo mara nyingi hutumia pikipiki kutekeleza uporaji.
Katika operesheni hiyo, pia risasi 27, bastola na risasi zake zilikamatwa.
Majambazi hao walikiri kuwa wamekuwa wakifanya uporaji sehemu mbalimbali kwa wapita njia.
No comments:
Post a Comment