Na Boniface Wambura, Marakech
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imetua mjini Marrakech, Morocco juzi usiku tayari kwa mechi ya kundi C kuwania tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya Morocco.
Mtanange huo umepangwa kuchezwa Jumamosi ya Juni 8, mwaka huu.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia hoteli ya Pullman ambayo pia ilikaa timu ya Ivory Coast ilipouja hapa kucheza na Morocco.
Kikosi hicho kimetua Marakech kikiwa na wachezaji 21, huku Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wakitarajiwa kuwasili jana mnamo saa nane mchana wakitokea Maputo, Msumbiji ambako timu yao ya TP Mazembe ilikuwa na mechi ya kombe la Shirikisho.
Katika mchezo huo, Stars ilitoka sare ya bila kufungana na Sudan ikicheza bila washambuliaji wake wake wawili nyota, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.
Kocha Kim Poulsen amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi vizuri na kitaimarika zaidi baada ya Samatta na Ulimwengu kujiunga na wenzao.
Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3:00 usiku kwa saa za Morocco, sawa na saa 5:00 saa za Tanzania.
Stars imewasili nchini Morocco ikitokea Ethiopia, ambako iliweka kambi ya wiki moja kwa ajili ya mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya FIFA uliochezwa Juni 2, mwaka huu dhidi ya Sudan kwenye uwanja wa Addis Ababa.
Katika mchezo huo, Stars ilitoka sare ya bila kufungana na Sudan ikicheza bila washambuliaji wake wake wawili nyota, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.
Kocha Kim Poulsen amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi vizuri na kitaimarika zaidi baada ya Samatta na Ulimwengu kujiunga na wenzao.
Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3:00 usiku kwa saa za Morocco, sawa na saa 5:00 saa za Tanzania.
No comments:
Post a Comment