Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mstaaf na Rais wa Zanzibar Mstaaf Dkt. Salmin Amour Juma, akizungumza na Wenyeviti wa CCM wa Mikoa sita ya CCM Zanzibar waliofika Nyumbani kwake kwa mazungumzo na kumsalimia mjini Migombani Unguja .
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, akitambulisha Ujumbe wa Viongozi wa CCM wa Mikoa ya CCM Zanzibar wakiti ulipofikwa kwa mazungumzo na Dkt. Salmin Amour maaruf wakati wa Uongozi wake akijulikana kwa jina la Komandoo.
Ujumbe wa CCM wa Wenyeviti wa CCM Mikoa sita ya Zanzibar , wakiwa katika viwanja vya nyumba ya Dkt. Salmin Amour.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa akitowa shukrani kwa niaba ya Wenyeviti wa CCM baada ya mazungumzo yao na Dkt. Salmin walipofika nyumbani kwake Migombani Unguja.
Dkt. Salmin Amour akiwa na Viongozi wa CCM wa Mikoa wakijumuika kwa kuitikia dua baada ya mazungumzo yao na Ujumbe huo uliofika nyumbani kwake migombani kwa mazungumzo.
DENNIS LONDO ACHUKUA FOMU YA UBUNGE MIKUMI
-
Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki aliyekuwa Mbunge
wa Jimbo la Mikumi, amechukuwa Fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Mikumi kwa
awamu...
1 hour ago
ndugu yangu kamandoo hali yako inatakiwa utubu kwa yale uliyoyafanya , vipi bado unajishughulisha na mambo ya kidunia , au unafikiri utaishi milele? hayo yaliyokufika bado hayatoshi kukumbusha ?
ReplyDelete