Mtume
Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:
:" إن في الجنة غرفة ..يرى ظاهرها من باطنها ، وباطنها
من ظاهرها ..أعدها الله لمن أطعم الطعام ، وألان الكلام ، وتابع
الصيام ، وصلى والناس نيام " رواه أحمد وحسنه الألباني
Hakika
peponi kuna vyumba, aliyeko nje humuona
aliye ndani na aliye ndani humuona aliye nje (transparent). Allaah ( Subhaanahu Wata’ala) Ameviandaa kwa wenye
kulisha watu chakula, wenye kusema kwa maneno mazuri na laini, wenye kuzifuatanisha
funga na wenye kusali ( usiku) ilhali
watu ( wengine ) wamelala
Imepokewa
na Ahmad na Sheikh Albaani amesema ni hadithi Hasan (nzuri)
Tunapolisha
na kuwakirimu waliofunga bila ya kufanya israafu wala kujionesha na kuwalisha
wale wanaoihitajia ( maskini na wasiojiweza na mayatima), tunapozungumza na
watu kwa maneno ya upole yaliyojaa hekima na busara ndani yake, tunapofunga kwa
kuziendeleza bila ya kuzikata kata au kuziacha mkono na tunapoamua kuamka usiku
mkubwa kwa ajili ya kusali tu na si vyenginevyo , haya ndiyo malipo ( jazaa)
aliyotuandalia Allaah Subhaanahu Wata’ala.
Tumuombe
Allaah Subhaanahu Wata’ala atuandalie vyumba hivyi kwa funga zetu tanozoendelea
kuzifunga na kwa ibada zetu za usiku tunazoendelea kuzitekeleza.
Aamiyn
No comments:
Post a Comment