Mtume
Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:
"رب
صائم ليس له من صومه إلا الجوع، ورب قائم ليس له من قيامه إلا السهر"
رواه النسائي
Ole
wake mwenye kufunga na asipate chochote katika funga yake isipokuwa (kukaa na)
njaa. Ole wake mwenye kusimama usiku (kwa ajili ya kusali) na asipate chochote
katika kusimama kwake isipokuwa kukesha tu
Imepokewa
na AnNasaaiy
Tunapozitekeleza
ibada zetu za funga na Ibada za usiku tuhakikishe tunakamilisha masharti ya
kukubaliwa ibada ambayo ni kuwepo kwa ikhlaas (kuifanya ibada kwa kutaraji
radhi zake Allaah Subhaanahu wata’ala pekee) wakati wa kuitenda amali yenyewe
na kisha kumfuata Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam wakati tunapoitekeleza.
Vyenginevyo amali hizi hazitopokelewa kama ni ibada na hivyo kupoteza muda wetu
tu.
Ewe
Mola, zikubali amali zetu za funga na Sala na ibada zetu nyengine kwani
tunazitekeleza kwa ajili ya kupata radhi zako tu.
Aamiyn
No comments:
Post a Comment