Na Ussi Talib
Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba Wilaya ya Kati Unguja, wamependekeza Katiba ijayo itamke rasmi kuwa mshirika wa Muungano ni Tanganyika na siyo Tanzania bara.
Maoni hayo yalitolewa jana huko Dunga wilayani humo mbele ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania inayongozwa na Mwenyekiti,Awadhi Ali Said.
Makame Ali Makame,alisema ikiwa Tanzania imekusudia kuondoa kero za muungano basi irudi katika uasilia wake wa nchi mbili huru zilizoungana ambazo ni Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar.
“Sawa na kukubaliana na mfumo mpya wa Muungano lakini Zanzibar iitwe hivyo na Tanganyika iitwe hivyo kama ilivyokuwa zamani” alisema Makame.
Pia aliitaka rasimu kila sehemu inayotaja Tanzania Bara itamke Tanganyika kwani kuweka kinyume na hivyo ni kumpa nafasi mmoja kujiona mkubwa.
Abuubakar Ussi Fadhili yeye alisema ni vyema kuweka uwazi huo ili kuondoa matatizo ambayo yanaweza kujitokeza.
Sambamba na hilo kwa upande wa Amin Yusouf Mussa mambo ya muungano yamependekezwa kuwa saba.
“Leo tunapendekeza mambo saba ya Muungano lakini Tanganyika haipo kama ikija kuyataka itakuwaje?”alihoji Mussa.
Akitoa ufafanuzi Mwenyekiti wa Kamati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Zanzibar,Awadhi Ali Said alisema,ili yatekelezeke hayo tume itaweka wazi shughuli za upande wa Tanzania bara ambazo zilikuwa zinashughulikiwa na Serikali ya Muungano na kuunda chombo chake kuyashughulikia.
Wajumbe hao wa Kamati ya mabadiliko ya Rasimu ya Katiba Mpya, wametawanyika katika sehemu mbalimbali kwa lengo la kukutana na wajumbe wa mabaraza ya Katiba walioteuliwa kuwakilisha wananchi ili kuunda Katiba Mpya itakayoleta mabadiliko ya mfumo na muundo mzima wa uongozi, watu na mamlaka husika kwa manufaa ya wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.
Chanzo - Mwananchi
A.alaikum
ReplyDeleteMbona hii habari ya zamani imechelewa kuwekwa hapa bwana othman ? Tunakuomba pia utuwekee maoni ya mabaraza ya katiba ambayo yanaendelea hapo zanzibar , sisi tulioko njee tunategemea kupata habari kutoka katika mitandao kama hii, lakini zaidi kwa sasa tunapata habari muhimu kutoka kwako.
SHukran
Ramadhan Kareem
Haya mawzo ya kuwa na jamhuri ya tanganyika huru yemedaiwa sikunyingi na mwenyekiti wa chama cha DP watanzania tulimzarau nakumbe alikuwa sahihi,sasakila konana ya zanzibar mnadai iwepo tanganyika, tumuungeni mkono mtikila, apate tanganyika yake na sisi tupate zanji yetu, acheni muamsho hawafanikiwi ulajimbele sawa na Cuf, hawatukomboi matumbombele,tumuungemkono mtikila kudai tanganyika yake
ReplyDeletesi kweli kumuunga mkono DP kuna manufaaa yoyote yale usisahau huyu ni mdini babu kubwa , tanganyika kuna watu wa dini mbili kuu si wote kina mtikila.
ReplyDeleteswala la jina la tanzania lina muunganisho wa majina TAN imetokana na TANganyika , na ZANIA imetoka ktk aZANIA yenye kumaanisha afrika kusini , babu ( nyerere) alikuwa haioni hasikii mbele ya afrika kusini na kuwapatia uhuru kwa hio jina tanzania liliwekwa ili kuonyehsa mshikamano wake na nchi za kusini mwa afrika , halina uhusiano wowote na zanzibar , mlidanganywa na babu