Habari za Punde

PBZ Yafutarisha Wateja wake na Wananchi wa Zanzibar.Bwawani.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar baada ya kuwasili katika viwanja vya hoteli ya Bwawani kuhudhuria futari ilioandaliwa na PBZ kwa Wateja wake na Wananchi wa Zanzibar.  

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ  Mwinyimbegu Jumbe na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Amour.





 Wananchi na Wafanyakazi wa PBZ wakijumuka na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, katika futari hiyo ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar.
 Wananchi wakipata futari wananchi katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Amour, akitowa shukrani kwa Wananchi waliohudhuria futari ilioandaliwa na benki yake katika Ukumbi wa Salama Bwawani na kuelezea mafanikio ya Benki hiyo kwa kutowa huduma kwa Wateja wake na kuzungumzia mikakati inayotarajiwa kufanyika katika kipindi hichi kwa kufunguwa matawi ya Benki katika Mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar ili kutowa huduma kwa wateja kwa ukaribu zaidi.  
 Wajumbe wa Bodi ya Benki ya Watu wa Zanzibar  wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Amour, akizungumza katika hafla hiyo ya futari, 
 Wananchi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Amour. akizungumza katika hafla hiyo ya futari kwa Wateja wa PBZ na Wananchi katika ukumbi waSalama Bwawani.
 Wananchi na Wafanyakazi wa PBZ wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ akitowa shukrani na kuzungumzia huduma zinazotolewa na Benki yake kwa wateja wa Zanzibar na nje ya Zanzibar.

 Kadhi Mkuu wa Zanzibar Khamis Haji Khamis akisoma dua baada ya kumalizika kwa dhifa ya futari iliandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd kwa Wateja wao na Wananchi wa Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Wananchi wakiitikia dua baada ya kupata futari ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.