Habari za Punde

Wataalamu wa India kuongeza nguvu kiwanda cha sukari Mahonda


Na Asya Hassan
WATAALAMU na wahandisi wengine wapatao 30 kutoka India wanatarajiwa kuwasili nchini wiki ya pili ya mwezi ujao kwa ajili ya kuungana na wenzao kuendelea na matengenezo makubwa katika kiwanda cha sukari Mahonda.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ifisini kwake Darajani, Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Krishinar Narayan alisema kufika kwa wataalamu hao kutakuwa chachu ya kukamilisha matengenezo ya kiwanda hicho na kuanza uzalishaji.

Alisema tayari wameagiza makontena 10 ya vifaa vipya ili kufungwa.

Alisema pamoja na kazi nyengine, wataalamu hao watakuwa na jukumu la kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wazalendo kuhusu uzalishaji wa sukari.

Aliiomba serikali kuunga mkono na kushirikiana na kiwanda ili kukiwezesha kufika lengo lililokusudiwa.

Alisema lengo la kiwanda ni kuhakikisha inaongeza kipato na inakuza uchumi kwa wananchi wa Zanzibar na inaondokana na uiagizaji wa sukari kutoka nje.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.