Habari za Punde

Bill Clinton Azinduwa Mradi wa Ondoa Malaria Zanzibar U






Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika uzinduzi huo wa Mradi wa kutokomeza Malaria Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya Amaan kwa mchezo wa mpira wa miguu uliozikutanisha timu za Veterani wa Zanzibar.
Rais Mstaaf wa Marekani Bill Clinto akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa kuondoa Malaria Zanzibar, wakati alipofanya uinduzi huo katika viwanja vya Amaan.
Rais Mstaaf wa Marekani Bill Clinto akisalimiana na refalii wa mchezo huo Hafidh Ali, aliochezesha mchezo huo, akifahamishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
Mtoto wa Bill Clinton akirusha shilingi kuashiria kuaza kwa mchezo wa uzinduzi wa Mradi wa Malaria uliofanyika uwanja wa Amaan uliozikutanisha timu za Wachezaji wa Zamani wa Zanzibar, uliofanyika katika uwanja wa Amaan.uliokutanisha timu za Jozani na Ngezi.
Mtoto wa Rais Mstaaf wa Marekani Chelsea akipiga mpira kuashiria kuzindua mradi wa kutokomeza Malaria Zanzibar, katika uzinduzi huo ulizikutanisha timu za Maveterani wa Zanzibar.
Kiongozi wa Timu ya Wazee Zanzibar Abdull Mshangama, akimkanidhi mlango wa Zanzibar Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinto, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Malaria Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa amaan.
Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinto akisalimiana na watoto wa moja ya timu za watoto zilizoandaliwa katika uzinduzi huo
Mtoto wa Bill Clinto Chelsea akisalimiana na wachezaji wa timu za watoto walioandaliwa katika sherehe hizo amaan.

Rais Mstaaf wa Marekani Bill Clinton na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, wakiangalia makablasha ya katika banda la kutolea damu.
Ofisa wa Mradi wa Clinto Foundation, akitowa maelezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Clinto na Mtoto wake Chelsea.wakiwa katika moja ya shamiana la kupimia malaria katika uwanja wa amaan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mgeni wake Rais Mstaaf wa Marekani Bill Clinton, kushoto Waziri wa Afya Juma Duni na kulia Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jidawi, wakiwa katika uwanja wa mpira Amaan, katika uzinduzi wa kuondoa kabisa Malaria Zanzibar ulizinduliwa na Rais Mstaadf wa Marekani kupitia Clinton Foundation.
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa Tokomeza Malaria Zanzibar uliofanyika viwanja vya Amaan

Wachezaji wa Timu za Veterani Zanzibar wakijumuika katika kutoa Damu kupima Malaria katika Uzinduzi wa Tokomeza Malaria Zanzibar uliozinduliwa na Rais Mstaaf wa Marekani Bill Clinton.
Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania na KMKM Shabani Ramadhani, akitowa damu kupima malaria katika uzinduzi wa mradi wa Ondoa malaria Zanzibar, uliozinduliwa na Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinton, katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Wananchi wakitowa Damu kupima Malaria katika viwanja vya Amaan Zanzibar.

4 comments:

  1. Mzee Clinton fanya ufanyavyo lakini usije ukawakabidhi njuluku smz, watazila halafu wakupige kamba malaria imekwisha huku wananchi wakifa kwa malaria, fatilia mambo yote kila kinotakiwa toa mwenyewe us, hao si binaadamu hapo

    ReplyDelete
  2. Ni kweli wala sio uwongo, SMZ si wa kupewa pewa, BIN CLINTON usije kujaribu hata siku moja kuwapa ile shilingi kumi smz wizi, hawana imani, njaa zao zipo kwenye matumbo yao, halafu hao wana vikampuni vyao uchwara vya kuchukua mikataba kazi utapeli, hawana lolote juu ya miradi smz.

    SMZ ina madudu mafisadi, Dr Shein ndio anae walea,akiambiwa anasema yeye hataki ushauri, yeye hamuogopi mtu,wala mungu wake, inatia imani sana kwa wananchi, maisha duni, malaria yanawateza, miundo mbinu mibovu, maji machafu kila kina ndio mazalio ya mbu,ikija mvua ndio balaa kubwa baadhi ya maeno ambayo yenye mabonde na kukaa maji.

    Nchi yetu zanzibar inaongozwa kinjaa njaa, viongozi hawana imani na wananchi, hawajawa tayari kuwaletea maendeleo,kutokana inaendeshwa kiurafiki, kisiasa, kiiitikadi, kiubaguzi, ya rabi tunakuomba uwabadilishe imani hawa viongozi wetu katika ramadhani tukubalie dua zetu ameen.

    Ghibuu

    ReplyDelete
  3. nafikiri mchangiaji wa mwisho nikusaidie , mwenyezi mungu hawabadilishi watu imani mpaka wabadilike wenyewe , dua ya kusema ni kumwomba atubadilishie atuletee viongozi bora wenye imani na uadilifu ,kama alivyokuwa nabii wake kipenzi alikuwa mtawala wa eneo kubwa ktk dunia , lakini alifariki hata mafuta ya kuwashia taa hamna nyumbani kwake , akifanya kazi zote za nyumbani mwenyewe hakuwa na walinzimwili( bodyguard) wala wafanyakazi wa nyumbani , hazina yote alikuwa chini ya mikono yake lakini hakuchua hata sarafu moja kwa manufaa yake au ya familia yake. Hawa viongozi tulionao ee mola uwaangamize na kuwalaani.

    ReplyDelete
  4. Napenda ZANZIBAR kuwa na mashirikiano

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.