Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud, akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa Zanzibar kuhusiana na matayarisho ya sherehe za Mapinduzi kutimia miaka 50, jinsi ya matayarisho yake na maandalizi yanayoendelea kufanyika kwa nyanja mbalimbali kuboresha Mapinduzi hayo kwa Uzinduzi wa Miradi Mbalimbali inayotarajiwa kufanyika.
Waandishi wa habari wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud, akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa Zanzibar kuhusiana na maandalizi ya sherehe za Mapinduzi kutimia mkiaka 50.mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamo wa Pili Vunga Zanzibar.
Viongozi wa Vyama vya Siasa vya Upizani Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud, alipokuwa akizungumza nao hkuhusiana na matayarisho ya sherehe za Mapinduzi kutimia miaka 50.
Nyie mnataka kuzihujumu hizo pesa tu mnakisherehekea nini hasa kwani mapinduzi yameleta faida gani hata mnasherehekea,munalazimisha mambo tu mimi sijaona faida ya Mapinduzi wala muungano situzinguwe hapa
ReplyDeleteUkataka usitake, mapinduzi na muungano yameleta faida kubwa kwa Zanzibar kisiasa, kiuchumi na kijamii.
ReplyDeleteInawezekana mwenzetu ni ktk Al-Basaid, ukoo uliopoteza ufalme wake 1964 lkn. hii haitaondoa ukweli kwamba sisi akina Machano, Jecha, Kijakazi nk. ni tofauti.
Inawezekana faida tunazozipata ni tofauti na zile tunazozitaka, lkn. 'ala kulli hali' tunashkuru, angalau ile dharau ya 'kimanga' imepungua!
Mimi hajiuliza, kamam sasa hivi ndugu zetu wenye asili za kiarabu wanatudharau kiasi hiki, haki ilikuwaje kwa wazee wetu enzi ya SAYYYID?
Mimi nadhani la muhimu hapa ni kulalamikia WAHADIMU wa SMZ namna wanavyotaka kuharibu PESA wakati hali ya HOSPITALI YA MNAZI MMOJA ni mbaya!