Na A K Simai
Niliwahi kuandika
takriban mwaka mmoja uliopita kwamba kulikuwa na matatizo katika ujenzi wa jengo
jipya la uwanja wa ndege katika makala yangu ‘Jengo jipya la uwanja wa ndege kunaini?’
Hivi karibuni kupitia
kwa Waziri mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundo mbinu alisema katika baraza
la wawakilishi wakati akiwasilisha bajeti ya makadirio na mapato ya wizara yake
na nanukuu:
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa ruhusa ya
kuendelea kwa ujenzi wa Jengo jipya la Abiria katika Uwanja wa ndege wa
Zanzibar lililosita kwa muda baada ya kuonekana kasoro za kiufundi
zilizojitokeza hapo awali katika jengo hilo.
Amesema katika kutekeleza hilo ujenzi huo umeanza
mara baada kukamilika kwa taratibu za Michoro mipya kwa baadhi ya sehemu za
jengo baada ya kupata Mshauri elekezi kutoka Nchini Ufaransa.
“Mnamo
mwezi wa Machi mwaka huu tulimpata mshauri elekezi na kuanza kazi mwezi April
na kutoa ripoti yake mwezi Juni mwaka huu ambavyo ilionesha namna ya kasoro
zilivyojitokeza na kuweza kutatuliwa haraka ipasavyo .”alisema Waziri Rashid
Seif.
Nikiwa kama
mwananchi na mkereketwa nimebakia tena na masuali yangu yale yale niliyoyaanika
mwaka mmoja uliopita na si vibaya kama nitayakariri kwani maelezo ya Waziri
hayajanipatia majibu ya kuridhisha.
Pia sikusikia
waheshimiwa wawakilishi wakitishia angalau kuzuia shilingi katika bajeti hii
mpaka wapate maelezo hatua gani zilichukuliwa dhidi ya watendaji waliopelekea
dosari hizi kutokea.
1. Ni timu gani iliyokuwemo katika kuandaa plan ya jengo hili ni watu
waliokuwa na uzoefu kwenye aviation au ni watu wa kuokoteza tu?
2. Hakukuwa na consultancy wakati wa kuandaa plan yenyewe na hakukuwa na kureview kuangalia kama kila kinachohitajika katika Airport ya kile kimewekwa?
3. Tulikurupuka katika kuingia mkataba huu ambao kwa sasa utaweza kutuingiza kwenye janga zito la deni lenye kuongezeka kwa riba pamoja na kuongezeka kwa gharama?
4. Kutakuwa na hatua zozote za kinidhamu au kuwajibika kwa waliotuingiza katika balaa hili au kulikuwa na mazingira ya ten percent?
2. Hakukuwa na consultancy wakati wa kuandaa plan yenyewe na hakukuwa na kureview kuangalia kama kila kinachohitajika katika Airport ya kile kimewekwa?
3. Tulikurupuka katika kuingia mkataba huu ambao kwa sasa utaweza kutuingiza kwenye janga zito la deni lenye kuongezeka kwa riba pamoja na kuongezeka kwa gharama?
4. Kutakuwa na hatua zozote za kinidhamu au kuwajibika kwa waliotuingiza katika balaa hili au kulikuwa na mazingira ya ten percent?
Jengo lilisimamishwa
mwezi July mwaka 2012 na tokea wakati huo Serikali ilikuwa ikihangaika kupata
mshauri mwelekezi na katika hatua hii iliwachukua miezi 9 kumpata mshauri
mwelekezi mwenye uweledi wa aina za kazi hizi. Well done Waziri kwa kulitatua
hili haraka ipasavyo.
Maelezo ya Waziri
hayaoneshi katika sehemu yoyote kwamba Serikali itawachukulia hatua za
kinidhamu au kuwawajibisha wale wote ambao walihusika kwa njia moja au nyengine
katika kuitia hasara kubwa Serikali hii na kuiongezea deni maradufu kwa kuombwa
mkopo wa ziada zaidi ya ule wa wa
US$ 70.4 milioni kutoka Exim Bank ya China.
Sijui interest rate yake ni kiasi
gani ila kulilipa hili itakuwa shughuli pevu kwani nilitarajia mhe Waziri
angalau angelitutajia ziada iliyoombwa kwenye mkopo huu ili nasi walipa kodi
tuanze kujiandaa.
Serikali haioni haja ya kuwawajibisha watendaji waliomtia aibu hata Rais
wetu wakati alipokuwa akikaguwa jengo hilo mwaka 2012 na kumhakikishia kwamba
litakamilka katika muda wake uliopangwa.
Dhana ya utawala bora inayosimamiwa na serikali haionekani kutekelezeka kwa
vitendo bali imebaki katika miongozo na kwenye semina elekezi tu?.
Mojawapo ya mipangilio ya utawala bora ni sera
ya uwajibikaji kutekelezwa kikamilifu kwa kila aliyekwenda kinyume na malengo
au maafikiano na dhamana alizokabidhiwa bila ya kuoneana muhali au kuchukuliana
baada ya kuthibitika kwamba ni kweli uzembe ulikuwa umetendeka.
Tunataka ushahidi gani tena
katika suala hili kama kulikuwa na uzembe?
No comments:
Post a Comment