Habari za Punde

Hadithi ya leo (15)



 

Mtume Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:

(( إن في الليل لساعةً لا يوافقها رجل مسلم يسأل الله تعالى خيرا من أمر الدنيا والآخرة إلا أعطاه إياه وذلك كل ليلة )) رواه مسلم

Hakika katika usiku kuna muda (saa)  endapo mja Muislamu atausadifu na kuupata (muda huo) huku akimuomba Allaah Ta’ala kheri za dunia na (tuendako) akhera basi (Allaah) humtakabalia na muda huo upo kila usiku

Imepokewa na Muslim

Hadithi nyengine inayotuhimiza kuuhuisha usiku kwa ibada hasa du’aa na si kwa kuitafuta laylatul Qadr pekee bali kwa kupeleka maombi yetu kwa Mola wetu mwenye kupokea na kusikiliza duaa zetu, vilio vyetu, shida zetu, mashtaka yetu zikiwa ni za kidunia na hata za kidini   .

Ramadhaan inatufundisha kuuhuisha usiku kwa ibada ya sala na kusoma Qur’aan pamoja na dhikr ( kumtaja Allaah Subhaanahu Wata’ala). Tudumishe kuhuisha huku hata baada ya Ramadhaan kila tukipata nafasi tukirudi kwa Allaah Subhaanhu Wata’ala katika wakati ambao wengine wamelala na Mola wetu Ameshuka hadi mbingu ya dunia akisubiri kusikiliza maombi yetu. Yeye Allaah ndie wa kuombwa.

1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.