Habari za Punde

PBZ Yakabidhi Vifaa vya Ujenzi Madrasa na Skuli Zanzibar kusaidia Jamii


Meneja Masoko wa PBZ Seif Suleiman, akimkabidhi Mabati 80 Ust Abdalla Ali Issa, kwa ajili ya Ujenzi wa Madrasa ya Marehemu Bimkubwa Staad Kisimamanjongoo. Unguja, makabidhiano hayo yamefanyika katika maeneo ya Muembeladu Unguja. PBZ husaidia Jamii kupitia faida inayoipata katika uendeshaji wa masuala ya Kibenki.  

Meneja Masoko wa PBZ Seif Suleiman, akimkabidhi Matofali 1900 Msaidizi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Miwani Wilaya ya Kati Unguja, kwa ajili ya ujenzi wa Madara katika Skuli hiyo 
Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Seif Suleiman, akimkabidhi matofali 2000 Ust. Idrisa Said wa Madrasatul Twuwa ya Mtoni Unguja kwa ajili ya Ujenzi wa Madrasa hiyo kutowa nafasi kwa wanafunzi wa madrasa hiyo kupata madrasa bora katika masomo yao ya Dini, PBZ hutowa misaada katika miradi ya Kijamii, kusaidi kupitia faida wanayopata na kuirejesha kwa Wananchi kusaidia jamii, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Mwanakwerekwe Unguja.

3 comments:

  1. Alhamdulillah tunashukuru sana

    ReplyDelete
  2. Alhamdulillah tunashukuru sana kwa msaada kutoka PBZ Allah awabarik
    Mlitupatia mabati hayo Chuo cha marehemu Maalim Bi mkubwa stadi

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.