Na Mwantanga Ame
UMOJA wa wanawake wa CCM mkoa wa kaskazini Unguja, umetakiwa kuondoa tofauti zao na kushirikiana ili kuhakikisha uandikishaji wa wapiga kura wapya katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa wanaCCM unafanikiwa. Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa huo, mama Asha Suleiman Iddi, aliyasema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa watendaji wa jumuiya hiyo katika ngazi ya shina, tawi na wadi yaliofanyika ofisi za wilaya ya CCM Mahonda.
Alisema suala la kuwa wamoja ni jambo la msingi na lazima waondoe tofauti zao ili kuhakikisha uandikishaji huo unakuwa na mafanikio.
Alisema CCM mara zote kinahitaji kupata ushindi katika chaguzi zinazofanyika nchini lakini hilo linaweza lisifikiwe ikiwa wanachama wataanza kutofautiana.
Alisema kwa kuwa uandikishaji wapiga kura wapya unatarajiwa kufanyika ndani ya wilaya hiyo kwa kuanzia katika jimbo la Kitope, kutahitajika nguvu ya pamoja ili kuona wanaostaki kuandikishwa wanapata fursa hiyo.
Mapema Katibu wa CCM wilaya kaskazini, Riziki Ahmeid Ali, alisema wanawake wa umoja huo wanapaswa kushirikiana kufanikisha zoezi hilo.
Nae Mbunge wa wanawake kwa mkoa huo, Bahati Ali, alimshukuru mama Asha kwa kuyafungua mafunzo hayo na kuselma ni ya msingi kwa awatendaji wa wilaya.
No comments:
Post a Comment