Na Kija Elias,Tanga
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amekiri kuwepo urasimu katika uwekezaji nchini tatizo ambalo linahitaji juhudi za pamoja kuliondoa.
Hayo aliyasema wakati akichangia mada katika kongamano la kwanza la uwekezaji kanda ya kaskazini linalofanyika jijini Tanga.
Alisema wapo baadhi ya viongozi wa serikali wamekuwa na urasimu pale mwekezaji anapotaka kuwekeza hali ambayo inawakatisha tamaa wawekezaji wengi.
Pinda alisema suala la urasimu katika uwekezaji bado ni changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo, ambpo aliwatka viongozi wanaohusika na sekta hiyo kuacha tabia ya kupokea rushwa ili kuwasaidia wawekezaji.
Alisema viongozi watakaobainika kupokea rushwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha tatizo.
Hata hivyo, alisema kumekuwepo na majukumu makubwa katika vituo vya uwekezaji, hivyo wanahitaji kugawa madaraka kuanzia ngazi za wilaya na mkoa ili kupunguza urasimu.
Mbunge wa jimbo la Kilindi, Beatrice Shelukindo, alisema suala la urasimu katika kupata maeneo ya uwekezaji bado ni tatizo kubwa kwa wawekezaji.
Aidha alisema kutokana na tatizo hilo atapeleka hoja binafsi bungeni ili ijadiliwe na hatimaye kupelekwa kwa wananchi.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Ameongoza Kikao cha 13 Cha Kamati Kuu ya
Taifa ya SENSA ya Watu na Mkaazi ya Mwaka 2022
-
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
akiongoza Kikao cha 13 cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi
ya Mwaka...
13 minutes ago
No comments:
Post a Comment