Na Khamis
Mohammed, Beijing
KUWEPO kwa vyombo
huru vya habari na vyenye kuzingatia maslahi ya umma, kumetajwa kusaidia kuinua
maendeleo ya kiuchumi na kijamii yaliopo hivi sasa nchini China ..
Profesa, alisema, pamoja na wajibu wa vyombo vya habari katika kuburudisha,
kuelimisha, kukosoa au kutetea, lakini pia vina wajibu wa kuhamasisha maendeleo
ya kiuchumi na kijamii kutokana na nafasi iliyonayo kwa taifa kwa kuzingatia
maslahi ya taifa.
Alisema, programu
za aina mbali mbali za kuelimisha jamii ya Wachina na dunia kwa ujumla
zimekuwa zikitayarishwa kupitia
telesheni ya taifa ya CCTV , hali ambayo imeweza kufikia wananchi wengi hata
wale walioko vijijini.
“China ina
magazeti 1943 ambapo magazeti 816 ni ya kila siku, ni fursa kubwa kwa wananchi
katika kupata habari”, alisema Profesa Yan.
Aidha, alisema,
mbali na wingi wa magazeti, China ina idadi
kubwa ya vituo vya televisheni vipatavyo 360 vikiwa na chaneli zaidi ya 2000
ambazo huangaliwa na watu zaidi ya milioni 900.
Akuzungumzia
rushwa kwa vyombo vya habari, Profesa Yan, alisema, China imekuwa ikipambana na aina
zote za rushwa na kwamba serikali ipo makini mno katika vita hivyo.
“Wapo watu
wameshahukumiwa mpaka adhabu ya kifo kwa kujishughulisha na rushwa na wengine
kutumikia viungo vya muda mrefu, hii yote ni kuonesha jinsi serikali
inavyokerwa na rushwa”, alisema.
Aidha, alisema,
vyombo vya habari vimekuwa vikifichua aina ya vitendo vya rushwa na kuitaja
kashfa ya maziwa yaliokuwa na sumu mwaka 2008, kwamba ilifichuliwa na vyombo
vya habari.
No comments:
Post a Comment