Mwanasiasa Mkongwe na Maarufu Zanzibar Balozi Isaac Abraham Sepetu amefariki dunia mjini Dar-es- Salaam juzi kwa ungonjwa wa Kiharusi.
Kwa taarifa iliopatikana kwa ndugu na jamaa zinaeleza kuwa marehemu alikuwa akisumbulia
na uongonjwa huu kwa muda miezi kadhaa, sasa alikuwa akiungua na kusumbuliwa na
maradhi ya kiharusi, pamoja na ungonjwa wa kisukari.
Marehemu Sepetu amefariki
juzi mjini Dar-es-Salaam.
Balozi Sepetu aliwahi
kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, katika miaka ya 1970, wakati wa
utawala wa awamu ya kwanza chini ya Rais Mwalimu Nyerere.Vilevile aliwahi kuwa
Balozi waTanzania nchini Urusitangu mwaka 1982 wakati wa utawala wa Mwalim
Nyerere.
Balozi Sepetu ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa juu
katika Serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serekali ya Mapinduzi
Zanzibar katika vipindi tafaiti
Marchi 27 mwaka huu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dkt. Ali Mohamed Shein, alimteuwa kuendelea na Uwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitegauchumi Zanzibar (ZIPA) wadhifa ambao
amekuwa nao hadi kifo chake .
Taarifa iliopatikana mipango ya mazishi inafanyika nyumbani
kwa marehemu maeneo ya Sinza Mori jijini Dar-es-Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa za jamaa zimeeleza kwamba mipango ya mazishi
itafanyika katika Kijiji chao Chuwini Wilaya ya Magharibi Unguja siku ya
jamatano na mwili wa marehemu utawasili Zanzibar
siku hiyohiyo na kuangwa katika kanisa la Minara miwili shangani.saa nne
asubuhi.
No comments:
Post a Comment