Habari za Punde

Dkt. Shein Aongoza Wananchi katika Mazishi ya Mdogo wake Rais Mstaaf wa Zanzibar Dkt. Salimin Amour.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimfariji Rais Mstaaf wa Zanzibar Dkt. Salmin Amour Juma, wakati wa maziko yake Kanal Mstaaf wa JWTZ Abuu Amour Juma huko katika kijiji cha Kidombo wilaya ya Kaskazini Unguja.   
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimfariji Rais Mstaaf wa Zanzibar Dkt. Salmin Amour Juma, wakati wa maziko yake Kanal Mstaaf wa JWTZ Abuu Amour Juma huko katika kijiji cha Kidombo wilaya ya Kaskazini Unguja.   
Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji watoto wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Dkt.Salmin Amour Juma, Papav Amini Salimin na Ndugu yake Mwinyi Salimn, wakati Makamo alipowasili katika kijiji cha Kidombo kwa mazishi ya Ndugu yake Rais Mstaaf wa Zanzibar Abuu Amour Juma. yaliofanyika kijiji kwao Kidombo Unguja.   
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Kabi, akiongoza sala ya kumuombea marehemu Abuu Amour Juma, katika msikiti wa Ijumaa Kidombo.katika sala hiyo imehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Rais Msataaf wa Zanzibar Dkt.Salmin Amour Juma na Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi na Viongozi wa Siasa na Wananchi. mbalimbali.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Kabi, akisoma dua baada ya kusalia maiti ya kumuombea marehemu Abuu Amour Juma, katika msikiti wa Ijumaa Kidombo.katika sala hiyo imehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Rais Msataaf wa Zanzibar Dkt.Salmin Amour Juma na Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi na Viongozi wa Siasa na Wananchi. mbalimbali.
Wananchi wakiitikia dua baada ya kumaliza kuusalia mwili wa marehemu Abuu Amour Juma katika msikiti waIjumaa Kidombo.
 Wananchi wakiwa wamebeba jeneza lilokuwa na mwili wa marehemu Abuu Amour Juma katika viwanja vya Kijiji cha kidombo.ikiwa tayari kwa mazishi. 
 Wapiganaji wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lilokuwa na mwili wa Marehe KanalMstaaf wa JWTZ Abuu Amour Juma, kuelekea katika eneo la kaburi kwa mazishi yake yaliofanyika kijiji kwao kidombo, wilaya ya Kaskazini Unguja.  

 Wananchi wakihudhuria mazishi ya Kanal Mastaaf wa JWTZ marehemu Abuu Amour Juma.katika kijiji cha kidombo Unguja wilaya ya Kaskazini Unguja.





 Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Tano Dkt. Salmin Amour Juma, akiweka mchanga kabri la ndugu yake marehemu Kanal Mstaaf Abuu Amour Juma. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi marehemu Kanal Mstaaf Abuu Amour Juma.
 Makamo wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Kanal Mstaaf Abuu Amour Juma.
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiweka mchanga kaburini.
 Rais Mstaaf wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Alhajjj Ali Hassan Mwinyi, akiweka mchanga katika kaburi.
 Wananchi wakiweka mchanga katika kaburi kukamilisha taratibu ya mazishi ya Kanal Mstaaf wa JWTZ Abuu Amour Juma katika kijiji chao kidombo. 
 Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Rais wa Tanzania Dkt.Mohammed Gharib Bilal, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, na Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi kutoka kushoto Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Tano Dkt. Salmin Amour Juma, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Juma Pembe na Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Kabbi, wakiitikia dua. 
 Wananchi wakiitikia Dua baada ya kumalizika kwa mazishi hayo huko kidombo.
  Wanafamilia na Wananchi wakiitikia dua baada ya kukamilika kwa mazishi ya marehemu Kanal Mstaaf wa JWTZ Abuu Amour Juma, yaliofanyika kijiji kwao kidombo Zanzibarv wilaya ya Kaskazini Unguja. 
 Kanal Shaban Lisu akisoma wasifu wa marehemu wakati wa uhai wake akiwa akilitumikia Jeshi la Wananchi Tanzania Marehemu Kanal Mstaaf Abuu Amour Juma. 
Kanal Shaban Lisu akimkabidhi risala ya wasifu wa marehemu Kanal Mstaaf wa JWTZ Abuu Amour Juma kwa kaka yake Rais Mstaaf wa Zanzibar Dkt. Salmin Amour Juma, baada ya kusoma wakati wa mazishi hayo yaliofanyika kidombo.kulia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,alihudhuria mazishi hayo na Viongozi wengine wa Chama na Serekali na Wananchi wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.