Habari za Punde

Pembea Duara (Great Wheel) , Seattle, Marekani

Miongoni mwa burudani za jiji la Seattle ni hili pembea duwara ambalo ni kivutio kikubwa kwa wageni na kwa wenyeji, watoto na watu wazima. 

Pembea hili limejengwa kando kando ya bahari na apandae hupata kuona mji vizuri. 

Zaidi ya hayo pembea hili ni kitega uchumi kikubwa kwa mji huu. Mpandaji hulipia dola zipatazo 20. 

Habari njema kwa wananchi wa Zanzibar ni kuwa pembea kama hili litawekwa katika kiwanja cha kufurahishia watoto cha Kariakoo. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii, ndugu Abdulwakil H. Hafidh, ambaye yupo ziarani hapa Seattle, pembea litakalowekwa Uwanja wa watoto wa Kariakoo litakuwa la kisasa zaidi pengine kuliko la Seattle. 

Ndugu Abdulwakil amewataka wananchi za Zanzibar kukaa mkao wa kula. Mohamed Muombwa Seattle, Marekani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.