Habari za Punde

Ngisi Jijini Seattle, Marekani

Mji hupambwa kama Bi Harusi ili uvutie. Jiji la Seattle mbali na kuwa na mishumaa mirefu ya majengo mazuri pia umepambwa na kazi nzuri za sanaa zenye uhusiano na mji wenyewe kama ngisi huyu anayeonekana kwenye picha. 

Kwa nini ngisi? Jiji hili limepakana na bahari ambapo ipo bandari kubwa. Sanaa hii inaonyesha uhusiano mkubwa uliokuwepo baina ya bahari na jiji. 

Mji wa Zanzibar ni mji wenye uhusiano na bahari. Kwa lugha nyengine umetegemea bahari katika uchumi wake. 

Ingependeza basi kama mji wetu unapambwa na sanaa zenye uhusiano na bahari kama pweza, ngalawa au kibua. Nchi kama binaadamu huendelea kwa kujifunza mambo mazuri kutoka nchi nyengine. 

Si vibaya kwa walezi  wa mji (baraza la manispaa) wetu kuanza kuiga au kuendelea kuiga mambo mazuri kwa ustawi wa mji wetu. 

Habari na picha kutoka kwa Mohamed Muombwa kutoka Seattle, Marekani

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.