مَنْ اغْتَسَلَ ثُمَّ أَتَى الْجُمُعَةَ فَصَلَّى مَا قُدِّرَ لَهُ ، ثُمَّ أَنْصَتَ حَتَّى يَفْرُغَ مِنْ خُطْبَتِهِ ، ثُمَّ يُصَلِّي مَعَهُ ، غُفِرَ لَهُ مَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجُمُعَةِ الأُخْرَى وَفَضْلُ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ ). رواه مسلم
Mtume Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam amesema:
Mwenye kukoga (josho la siku ya Ijumaa) kisha akasali kadri ya alivyojaaliwa (kusali Sunna), kisha akanyamaza (kusikiliza khutbah) mpaka Khateeb (Imam) atakapomaliza khutbah yake, kisha akasali naye, husamehewa madhambi yake tokea wakati huo hadi siku ya Ijumaa inayofuatia na ziada ya siku tatu pia ( atasemehewa madhambi yake). Muslim
Hadithi hii inatufundisha fadhila na umuhimu wa Sala ya Ijumaa kwa kila Muislamu. Inatuelekeza kukithirisha ibada siku ya Ijumaa hasa Sala kwa kuwahi msikitini mapema na kusali kadri ya tutakavyojaaliwa na huku tukihakikisha tuna utulivu kwa kunyamaza kimya hasa pale Imam anapokhutubu na kusali pamoja naye.
Fadhila zake ni kusamehewa madhambi yote madogo madogo ( kama ilivyokuja katika riwaya nyengine) na Allaah Subhaanahu Wata’ala ametupa bonus ya kutuongeza siku tatu zaidi
No comments:
Post a Comment