Habari za Punde

Wastaafu ZBC waagwa

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC Yussuf Khamis (Mwenye shati la drafti katikati) katika picha ya pamoja na WafanyakaziWastaafu wa ZBC walio mstari wa mbele, katika Hafla maalum ya kuwaanga iliyofanyika Bungi Mkoa wa Kusini Unguja. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

NA MAELEZO ZANZIBAR     

Wastaafu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC wametakiwa kutoa ushirikiano wao pale unapohitajika ili kulifanya Shirika hilo kuzidi kusonga mbele.

Wito huo umetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Yussuf Khamis katika Hafla maalum ya kuwaanga Wafanyakazi Wastaafu wa Shirika hilo iliyofanyika Bungi Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema licha ya Wastaafu hao kuwa nje ya kazi ushauri wao utazingatiwa ili kuliimarisha zaidi Shirika hilo.


“Nakuombeni musijitenge moja kwa moja na Shirika kama mna ushauri wowote basi karibuni Ofisini ili kuliendeleza Shirika letu ”

Aidha Yussuf amewataka Wafanyakazi wa ZBC kuzidisha mashirikiano miongoni mwao ili kurahisisha utendaji kazi wa kila siku.

Kwa upande wao Wastaafu hao waliushukuru uongozi wa Shirika kwa kuweza kuwaandalia Hafla maalum ya kuwaaga jambo ambalo walidai baadhi ya taasisi hawafanyi hivyo.

Aidha waliiomba Serikali kuzidi kuyaboresha maslahi ya Wafanyakazi ili Wanapomaliza muda wao wa kulitumikia taifa waweze kumudu maisha yao vyema.

Katika Hafla hiyo Jumla ya Wafanyakazi Wanne waliagwa na kukabidhiwa zawadi baada ya muda wao wa Utumishi kumalizika.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.