Habari za Punde

Nahodha: 'Mimi ni mtetezi wa suala la mafuta na gesi liondolewe kwenye Muungano'

 Waziri Mstaafu wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Mhe Shamsi Vuai Nahodha alipokuwa akizungumza na WanaCCM kwenye jengo la Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Amani jana.
 
Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha amesena anaungana na kundi la wazanzibar wanaotaka Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ndani ya katiba ijayo ya jamhuri ya muungano Tanzania.
 
Akizungumza na wanachama na viongozi katika ofisi za CCM mkoa wa mjini kichama amesema katika baadhi ya maeneo ya kuendesha nchi suala la mamlaka kamili ni muhimu kuimarisha uchumi wa Zanzibar.
 
Nahodha aliewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa amedai yeye ni mtetezi wa suala la mafuta na gesi liondolewe kwenye muungano.
 
Hata hivyo amesema anashangazwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaodai sarafu ya Zanzibar, kiti cha umoja wa mataifa na wizara ya ulinzi akidai masuala hayo yanahitaji gharama kubwa za uendeshaji.
 
Aidha Nahodha amesema wakati Zanzibar ikiendelea kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduziu Zanzibar muungano utaendelea kubaki uti wa mgongo wa maendeleo ya ulinzi na usalama wake.

Amesema licha ya mfumbo wa muungano wa serikali mbili kujaa matatizo, lakini njia ya kuyapatia ufumbuzi ziko huru  badala ya kun'gan'gania  muungano wa mkataba au serikali tatu akidai haiku salama na Zanzibar

Chanzo: Zanzibar Islamic news blog

4 comments:

  1. Bado nashindwa kumfahamu. Anasema anaungana na wazanzibari kwa mamlaka kamili. Halafu anapinga kwa kusema haungi mkono Serikali tatu na muungano udumu. Jaje mwanakele!!!.

    ReplyDelete
  2. Nahodha nafikiri bado anajaribu kutaka kuwavuta watu na ndoto zake za urais na ndio maana leo anazungumza hivi ingawa pia anajizonga tuu, mimi nafikiri hiyo ndoto ya urais aondoshe kabisa , labda abebwe na CCM, lakini tokea hapo mwanzo hana mvuto wa kisiasa si zanzibar wala bara. Hata uwezo wake wa kuendesha nchi umetawaliwa na chuki na ubaguzi. Siku za karibuni kabla ya kufukuzwa uwaziri alikuwa ndio miongoni mwa wachochezi wakubwa wa ubaguzi wa upemba na uunguja. MOla atuepushe na kiongozi wa aina hii, ambae tokea alfajiri ameshaonesha dalili za wazi za kushindwa kusimamia majukumu ya kuongoza Umma.

    ReplyDelete
  3. Nahodha bado hujaeleweka, unaongea hayo kwakua umefukuzwa na Kikwete? Mimi nampongeza Mhe Rais kwa maamuzi yake bila shaka amegundua mapungufu kwako

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.