Na Mwashamba Juma
WAKATI Zanzibar inaadhimisha
miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, lugha ya kiswahili imezidi kuimarika na
kukua kutokana na juhudi zinazochukuliwa na sekali ya kuieneza lugha hiyo.
Katibu Mkuu wizara ya habari,utamaduni,utalii na michezo, Dk. Ally
Saleh Mwinkai, aliyasema hayo wakati akifungua kongamano la Kiswahili
lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika kampasi ya
chuo hicho,Beitras.
Alisema juhudi za serikali ya Zanzibar kukiimarisha kiswahili zilianza
tokea mwaka 1964 baada ya rais wa kwasnza wa Zanzibar kutangaza kiswahili
kitumike kama lugha rasmi katika shughuli za serikali.
Alisema katika kutekeleza juhudi hizo taasisi mbalimbali za kusimamia
na kukienzi kiswahili kwa wakati huo ziliundwa zikiwemo Baraza la kiswahili,
Baraza la sanaa, Idara za kiswahili katika vyuo vikuu na kituo cha kimataifa
cha uatafiti na uendelezaji wa lugha ya kiswahili.
Alisema juhudi hizo kwa sasa zinaendelea baada ya kuanzishwa Kamisheni
ya kiswahili ya Jumuiya ya Afriaka Mashariki ambayo ofisi zake zipo Zanzibar.
“Hapana shaka juhudi zinazochukuliwa na serikali ya SMZ zimeleta
mafanikio makubwa miongoni mwao ni kukilea kiswahili sambamba na kuongeza
wataalam katika ngazi zote za taaluma,” alisema.
Alisema kukua kwa kiswahili ni kuongezeka misamiati na matumizi ya
kijamii, utamaduni, mazingira, sayansi na teknolojia pamoja na kutanuka
kisarufi.
Alisema katika kipindi hiki cha kuadhimisha miaka 50 ya
Mapinduzi,idadi ya waandishi wa vitabu vya fasihi na lughawiya hasa katika
tanzu za mashairi, riwaya na tamthilia, imeongezeka ikilinganishwa na miaka ya
nyuma na sasa vinatumiaka katika taasisi mbalimbali za taaluma za ndani na nje
ya Zanzibar.
Hata hivyo, alisema kuna baadhi ya wasomi hukipotosha na kukitumia
vibaya kiswahili kwa kubuni maneno yasiyolingana na ufasihi unaostahiki.
“Kuna matumizi ya maneno yanachefua nyoyo kwa watambuzi wa lugha ya
kiswahili wanapoyasikia yakitamkwa, cha kutisha ni kwamba wanaofanya hivyo ni
wataalamu wetu na kwenye vyombo vyetu vya habari,” alisema.
Alisema hali hiyo haikiimarishi kiswahili bali inakipotosha na
kurudisha nyuma juhudi za serikali kukikuza na kukiimarisha.
Alisema kuna haja ya kuendelea kuimarishwa kiswali kwani kila
kinachokua hulazimika kuimarishwa ili kisife kama ilivyo kwa kiswahili.
Aidha alisema wasomi wengi hupendelea kutumia lugha za kingeni
wanapokuwa kwenye mihadhara ya watu, warsha au makongamao, kwani wengi huona
hawatotambulika kuwa wasomi, matokeo yake hukiacha kiswahili kitumike mitaani
na baadhi ya sehemu za kazi.
Alisema jamii ina jukumu la kukienzi na kujivunia lugha yaona na wawe
tayari kukizungumza mahala popote bila kuona aibu.
Barani Afrika kiswahili kinazungumzwa zaidi katika ukanda wa Afrika
Mashariki zikiwemo Tanzania, Kenya,Uganda, Burundi,Rwanda, na Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo kwa Afrika ya
Kati.
No comments:
Post a Comment