MENEJA wa kiwanda
cha Mafuta ya Makonyo Wawi Chake Chake Pemba, Ramadhan Kombo Feruzi akizungumza
na ujumbe wa waandishi wa habari kutoka tanzania bara ba Zanzibar, wakati
walipofanya zaiara yao ya kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo katika
kiwanda hicho.
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
MKUU wa ghala la
makonyo lililomo ndani ya kiwanda cha makonyo wawi Chake Chake Pemba, Hamad
Said Omar, akiwaonyesha waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya
habari Tanzania bara na Zanzibar, makonyo gredi ya kwanza. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
INJINIA wa
mtambao wa kisasa wa kuangalia ubora wa mafuta ya Mimea uliomo ndani ya kiwanda
cha Makonyo wawi Pemba, Anton Pretorius akitoa maalezo kwa waandishi wa habari
kutoka vyombo mbali mbali vya habari Tanzania bara na Zanzibar walipotembelea
kiwanda hicho. (Picha na Abdi Suleiman,
Pemba.)
MSAIDIZI meneja
wa kiwanda cha Makonyo wawi Chake Chake Pemba, Hamadi Ali Mohamed,
akiwafahamisha waandishi wa habari kutoka Vyombo mbali mbali vya habari
Tanzania bara na Zanzibar, juu ya mashine ya ufikichaji mafuta ya makonyo
inavyofanya kazi wakati walipotembelea kiwanda hicho. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
MSAIDIZI meneja
wa kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba, Hamad Ali Mohamed,
akiwafahamisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari, kutoka
tanzania bara na Zanzibar, juu ya mtambo wa kiwanda cha kukamulia mafuta ya
makonyo unavyofanya kazi. (Picha na Abdi
Suleiman, Pemba.)
WAANDISHI wa
habari kutoka vyombo vya habari Tanzania bara na Zanzibar, wakiangalia jiwe la
msingi la kiwanda cha makonyo, lililowekwa na marehemu rais wa Mwalimu Julias
Kambarage Nyerere mwaka 1982. (Picha na
Abdi Suleiman, Pemba.)
MWANDISHI wa
habari kutoka Habari Maelezo Pemba, Maruzuk Khamis akiangalia gredi ya kwanza
ya makonyo safi, katika kituo cha ununuzi wa karafuu Mazambarauni Wilaya ya
Wete, wakati wa ziara ya waandishi wa habari, kutoka vyombo vya habari Tanzania
bara na Zanzibar. (Picha na Abdi
Suleiman, Pemba.)
WAANDISHI wa
habari kutoka Vyombo mbali mbali vya habari Tanzania bara na Zanzibar,
wakizungumza na mkulima wa karafuu, katika kituo cha ununuzi wa zao hilo,
mazambarauni Wete wakati wa ziara yao. (Picha
na Abdi Suleiman, Pemba.)
MKULIMA wa zao la
karafuu katika kijiji cha Mtambwe akitandaza karafuu zake katika turubali, ili
zikikauka kuziuza katika kituo kipya cah ZSTC Mtambwe, kilicho zinduliwa na Mhe
dk Ali Mohamed Shein wakati alipofanya zaira yake kisiwani Pemba. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
MHANDISI mkaazi
wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba, Khamsi Mosuod Khamis akitoa
ufafanuzi wa ujenzi wa barabara 5 za kisasa kwa kiwango cha lami, mkoa wa kaskazini
Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
GARI la kampuni
ya H young likishindilia kokoto levuli ya mwisho katika barabara ya Kipangani
hadi kangagani, ikiwa ni moja kati ya barabara tano za mkoa wa kaskazini Pemba.
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
GARI maalumu la kampuni
ya H young,likitandaza kokoto baada ya kumwaga lami babarani,ikiwa ni hatua ya
mwisho kukamilika kwa barabara, kama linavyoonekana katika picha. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
GARI la kubebea
mizigo la kampuni ya H young likimimina kokoto katika gari maalumu ya kutandaza
kokoto barabarani, katika barabara ya kipangani hadi kangagani, miongoni mwa
barabara tano za mkoa wa kaskazi Pemba,kama linavyoonekana katika picha. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
No comments:
Post a Comment