Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Kombe la Mapinduzi Nahodha wa Timu ya Kcc kutoka Uganda Kawoya Fahad,katika mchezo wa Fainali na Timu ya Simba,uliochezwa lao katika uwanja wa Amaan Mjni Zanzibar ikiwa sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi,katika mchezo huo Kcc ilifunga Simba kwa bao 1-0.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk, akimkabidhi Kombe la Mshindi wa Pili wa Michuano ya Mapinduzi Cup timu ya Simba Nahodha wa Timu hiyo Ivo Mapunda, baada ya mchezo wa fainali kumalizika kwa timu ya Simba kufungwa Bao 1--0
Vikosi vya Timu ya Simba na KCC wakiingia uwanjani kutimiza Fainali ya Mapinduzi Cup mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan na timu ya KCC ya Uganda imeshinda mchezo huo kwa bao 1--0
Mashabiki na Wapenzi wa timu ya Simba ya Dar-es-Salaam wakishangilia timu yao wakati wa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi, mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia wachezaji wa timu ya Simba kabla ya kuaza kwa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia wachezaji wa timu ya KCC kabla ya kuaza kwa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan.
Kikosi cha Timu ya KCC ya Uganda kilicholinyakuwa Kombe la Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. katika mchezo wa fainali baada ya kuifunga timu ya Simba kwa Bao 1--0
Kikosi cha timu ya Simba kilichokubali kufungwa na Timu ya KCC ya Uganda katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa na Vingozi wa Serekali wakifuatilia mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi 
No comments:
Post a Comment