Habari za Punde

Maalim Seif safarini Afrika Kusini

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia mmoja kati ya mikutano ya Kimataifa. (picha na OMKR)

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameondoka nchini leo kuelekea Afrika Kusini kwa ziara ya siku mbili ya kisiasa.

Akiwa nchini humo Maalim Seif atashiriki katika mkutano mkuu wa muungano wa vyama vya kileberali na democrat vinavyojumuisha baadhi ya nchi za Ulaya, Pacific, Afrika na Caribbean.

Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mjini Capetown, Maalim Seif akiwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, anatarajiwa kupata fursa ya kuwasilisha hotuba yake kwenye mkutano huo.
 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.