Habari za Punde

MAHMOUD THABIT KOMBO KUUNGURUMA LEO KWENYE MKUTANO WA HADHARA –BUYU PWANI.

Na Andrew Chale, Zanzibar
CHAMA cha Mapinduzi CCM, leo Januari 24, kinatarajia kufanya kampeni yake ya tatu ya mkutano wa hadhara kwenye eneo la Buyu Pwani, katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa  Jimbo la Kiembesamaki,  ambapo mgeni rasmi wa kumnadi Mgombea anatarajiwa kuwa, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Jumuiya ya CCM (UVCCM)  na  (MNEC), Ndugu.  Shaka Hamdu Shaka.

Akielezea mkutano huo wa tatu wa hadhara, unaotarajiwa kuwa majira ya Saa kumi jioni, eneo hilo la Buyu- Chukwani, Mahmod Thabit Kombo , aliwaomba wananchi wa Buyu kujitokeza kwa wingi ilikumsikiliza na kuzijua sera za Chama katika kuwaletea maendeleo.

“Leo Januari 24, nawaomba  wananchi wa Buyu, kujitokeza  kwa wingi ilikusikiza sera , Ilani na mipango endelevu tuliyojipangia ndani ya chama” alisema Mahmoud Thabit Kombo.

Aidha, aliwaomba wananchi wa Buyu, ifikapo Februari Mbili, siku ya Jumapili, wampigie kura ya NDIYO, ilki awe Mwakilishi wao atakayeenda kuwatetea kwenye Baraza la Wawakilishi, sambamba na kumaliza kero zinazowakabiri.

Baadhi ya mambo, mbalimbali anatarajia kuzungumzia ikiwemo kero za maji, elimu, kuwezesha vijana, akinamama na jamii nzima ya jimbo hilo la Kiembesamaki, pindi watakapomchagua.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.