Habari za Punde

CCM Jimbo la Kiembesamaki Yaibuka na Ushindi wa Asilimia 75.1

Na Mwandishi Wetu
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameibuka Kidedea kwa ushindi alioupata katika uchaguzi huo mdogo wa Jimbo hilo baada ya kukaa wazi kwa muda mrefu kutokana na kutenguliwa kwa aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.

Masimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki Ndg. Suluhu Rashid , akitangaza matokeo hayo baada ya kumalizika kwa kazi ya uhesabuji wa Kura na kuzijumlisha kura zote zilizopingwa na Wananchi wa Jimbo hilo.

Akitangazo matokea hayo ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki  yalioshirikisha Vyama Sita vya Siasa vilivyosimamisha wagombea wake.

Msimamizi wa Uchaguzi Ndg. Suluhu akitoa matokeo hayo Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameshinda kwa  Kura 1856, sawa na asilimia 75.1 na kutangazwa mshindi wa Uchanguzi huo Mdogo wa jimbo hilo kuchukuwa nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Mansoor Yussuf Himid, aliyevuliwa Uwanachama na CCM na nafasi hiyo kuwa wazi kwa muda hadi kufanyika kwa uchaguzi mdogo leo na kumpata mrithi wa kiti hicho.


Mgombea wa Chama cha CUF Mhe. Abdulmalik Juma Jecha, amepata kura 445, sawa na asilimia 18.3, Mgombea wa Chama cha ADC Mhe. Amani Ismail Rashid  amepata kura 84, sawa na asilimia 3.5, Chama hichi ni kipya kimeungwa na Viongozi walioondoka CUF, na hii ni mara ya pili kushiriki Uchanguza tangu kuazishwa kilishiriki uchaguzi wa kwanza kisiwani Pemba katika jimbo la Chambani,Pemba.

Nae Mgombea wa Chama cha  CHADEMA Mhe. Hashim Juma Issa,amepata kura 34 sawa na asilimia 1.5, katika uchaguzi huo mdogo wa jimbo la kiembesamaki.Mgombea wa TADEA Ali Mohammed Ali (Mbongo) amepata kura 6 sawa na asilimia 0.3. Nae Mgombea wa Chama cha SAU Mhe. Ramadhani Simai Mwita amepata kura 1 sawa na asilimia 0.1

Kwa matokeo hayo Tume ya Uchaguzi Zanzibar imemtangaza Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kuwa ni Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki na anakuwa Mwakilishi halali baada ya ushindi huo.


  


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.