Habari za Punde

Kikao cha Bunge Maalum la Katiba Kuanza Leo Mchana kwa Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa Bunge.

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na  Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya  Muungano wa Tanzania  Dkt. Thomas Kashillah amesema Kikao cha Bunge hilo litaanza kwa hatua ya kumchagua Mwenyekiti wa Muda wa Kikao hicho kwa ajili ya kupanga kanuni za kuendesha Kikao na kufanya uchaguzi 

Amesema  katika uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa Bunge atapigiwa kura na wajumbe na Makamo Mwenyekiti wake, ili kuanza kwa  kuendesha Kikao cha Bunge la Maalum la Katiba Mpya ya Tanzania kupitia Rasimu ya Pili ya Katiba hiyo ili kuichangia na kupata Katiba iliokuwa Safi 

Amesema Kikao hicho kitakuwa chini ya Katibu  wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Yahya Khamis Hamad , na kufanya uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa Muda wa Kikao hicho

Amesema taratibu zote za Kikao hicho zimekamilika na kinachusubiriwa ni kuanza kwa Kikao hicho cha Historia kwa Tanzania kupitisha kwa Katiba ya Tanzania ni mabadiliko ya Kwanza tangu Tanzania kupata Uhuru.
Tayari takribani  Wajumbe wate wa Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania Wameshawasili Mkoani Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Bunge la Katiba Tanzania.

Mji wa Dodoma ukiwa katika uchangamfu wa wageni mbalimbali waliofika kushuhudia mkutano huo wa historia kwa Tanzania kupitisha Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wananchi wa Tanzania wataangalia Bunge hilo Maalum kupitika katika Vyombo vya habari mbalimbali Tanzania na kuoneshwa katika TV ya Taifa ya TBC, na Tv nyegine wakati wa saa nane mchana zitakapoaza shughuli hizo leo huko Dodoma. 

1 comment:

  1. Ongereni sana wajumbe wa katiba mpya, nawasihi enyi wajumbe wekeni mbele masilahi ya utaifa wetu nasi ushabeki wa vyama, utatuponza na bahati nzuri JK alisema kwa kutoa angalizo. Pitieni kipengere hadi kipengere na kubaini mapungufu ili yalekebishwe. napendekeza swala la muungano ambalo lingonga vichwa vya walowengi isiwe dili sana, yapo matatizo rufufu mbali na muungano ambayo kwayo yasipojadiliwa kwa kina tz yetu inapotea, mfano, kumiliki mali kwa viongozi wa juu huku watz wakilalama na umaskini, mamlaka ya wananchi kumkataa na kumshtaki mbunge endapo watapoteza imani nae,

    muungano, maoni yangu nataka selikali moja tu wala si mbili au 3, watanganyika na wazanzibar ni wamoja, tukijitenga kutaibuka sis ni watangnyika na sisi ni wazanzibar, hapo hapo ndani ya watanganyika kutakuwa na ukabila, dhambi kubwa hiyo itatutafuna.

    pia katiba mpya iweke bayana jinsi ya kutumia na kurejesha fedha za wahisani, si kila mwaka tunaongeza deni la taifa, ambalo kwa sasa linatishia wengi (til. 27).

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.