Habari za Punde

Mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soko Bara la Afrika Chuoni na Howmine Imeshinda 2--1

Bendera za Vyama vya Mpira na Nchi washiriki wa michuano hiyo zikipepea wakati wa mchezo huo, kati za Chuoni na HowMine
Viongozi wa Vyama vya Mpira Barani Afrika wakifuatilia mchezo huo.
                 Beki wa timu ya Chuoni akimkata mtama mchezaji wa timu ya HowMine ya Zimbabwe.
              Mshambuliaji wa timu ya How Mine akijaribu kuwapita wachezaji wa timu ya Chuoni
  Mashabiki wa jukwaa la Urusi wakishangilia mchezo huo kwa staili ya aina yake kwa kupuliza mavuvuzela
Beki wa timu ya Chuoni akimzuia mshambuliaji wa timu ya How Mine, timu ya How Mine imeshinda 2--1 mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan.




Wachezaji wa timu yaHow Mine wakishangilia goli lao la kusawazisha lililopatikana katika dakika ya 27 ya kipindi cha kwanza lililofungwa na mchambuliaji wake Sibandwa, katikati akishangilia golilake nje ya uwanja wa amaan.




Mchezaji wa Chuoni na wa Howmine wakikimbilia mpira katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika,mchezo uliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar, timu ya HowMine imeshinda 2--1 
Mshambuliaji wa timu ya Chuoni akijaribu kumpiga chenga kipa wa timu ya Howmine ya Zimbabwe, katika mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya Howmine imeshinda 2--1  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.