Na Kija Elias, MWANGA
MTU mmoja amefariki dunia huku wengine 16,
wakijeruhiwa vibaya, baada ya basi la
kampuni ya Hood lenye namba za
usajili T.488 AXV aiana ya Scania kupata ajali mbaya, majira ya saa 3:00 asubuhi katika barabara ya
Same- Mwanga, wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro,
Robert Boaz, ajali hiyo imesababishwa na kupasuka tairi ya mbele na hivyo
kusababisha basi hilo kukosa mwelekeo na kuanguka.
Alisema katika ajali hiyo aliyefariki ametambulika
kwa jina la Joshua Likumbia (45),raia wa
Kenya, ambaye alikuwa akisafiri kuelekea jijini Mbeya.
Alisema kati ya majeruhi 16, yupo pia dereva wa
basi hilo, Fadhili Hashim, ambae amelazwa hospitali ya wilaya ya Same, huku
wengene wakitibiwa hospitali ya rufaa (KCMC) ambapo wanane kati yao hali zao
sio nzuri.
Aliwataka madereva kuwa waangalifu wawapo
barabarani ili kuepuka ajali zisizo za lazima.
No comments:
Post a Comment