Na Joseph Ngilisho,ARUSHA
KANISA la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), limewaonya
wake wa watumishi wa kanisa hilo kuacha kuvaa nguo za kubana na zinazoacha wazi
sehemu kubwa ya miili yao kwa sababu kitendo hicho ni ukiukaji wa maadili ya kanisa.
Kauli hiyo ilitolewa na Askofu wa Kanisa hilo,
kanda ya kaskazini, Martin Shao, kwenye ibada maalumu ya kumtawaza mchungaji
mpya wa kanisa hilo, Godlisten Wilison Mkenda, kuingia daraja la uchungaji,iliyofanyika
kanisa la KKKT usharika wa Salei jimbo kuu la Arusha.
Alisema watumishi wa mungu wamekua na changamoto
kubwa katika kutoa huduma kwa waumini na muda mwingine inasababishwa na
wachungaji wasiokua na imani ya kutosha kwa kushindwa kuyakabili majaribu
kutokana na vishawishi.
Alisema pamoja na changamoto hizo, wakati mwingine zinachangiwa
na baadhi ya wake wa watumishi na waumini kwa kuvaa nguo zisizofaa na kuwaingiza watumishi katika majaribu.
Alisema wake wa watumishi wamekuwa wakishindana na
mambo ya kidunia na kusahau kuwa wao ndio kioo cha jamii na wanapaswa kuwa na maadili
mema.
Alisema Wakristo watambue kuwa majaribu yapo kwa
kila binadamu lakini anayo nafasi ya kukabiliana nayo na kuyashinda,na kwamba
yapo majaribu mengine ambayo umfanya mtu
kukomaa na hatimaye kupata ushindi wa uzima.
Aidha aliwataka watumishi wa serikali na siasa
kulifuata neno la Mungu kwani wanakumbana na majaribu makubwa maofisi na wakati
mwengine yanawashinda.
Kwa upande wake, Mchungaji Godlisten Mkenda,
aliseam anamshuku Mungu kwa tukio hilo kwani ni malengo yake ya siku nyingi kuwa
mchungaji.
No comments:
Post a Comment