Na Fatma Kitima, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Hesabu za Serikali ya Bunge (PAC),
imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuafanya
ukaguzi maalumu wa suala zima IPTL na uhalali wa utoaji wa fedha kutoka akaunti
maalumu ya Tegeta Escrow.
Aidha Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) imetakiwa kuanza uchunguzi wa
mchakato mzima wa mkataba wa IPTL, umiliki wa kampuni hiyo na uhamishaji wa
umiliki kwenda kampuni ya PAP.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe, alisema
hayo baada ya kuzungumza na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupokea maelezo
kuhusu fedha shilingi bilioni 201 za akaunti ya Tegeta Escrow.
Alisema Kamati imeshangazwa na kitendo cha Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini kuanzisha ukaguzi maalumu wakati yeye mwenyewe ni
mtia saini kwenye hati ya kutoa fedha hizo na mshiriki mkubwa katika mchakato
mzima.
Hivyo, kamati imeagiza ukaguzi maalumu kutoka
kamati PAC ili kuweza kupata ukweli.
Zitto alisema PAC imetoa mpaka mwisho wa mwezi Aprili
taarifa ya ukaguzi huo iwe imekamilika na kuwataka wahusika wote wa mchakato wa
IPTL kusubiri matokeo ya ukaguzi.
Alisepa
pia PAC imetaka maamuzi ya mahakama kuheshimiwa.
Alisema Kamati ina wasiwasi kwamba TANESCO, kwa
mujibu wa nyaraka, itatakiwa kulipa fedha nyingi zaidi zinazofikia zaidi
shilingi 200 bilioni kwa kampuni
iliyonunua IPTL.
Akizungumza na waandishi wa habari, Gavana wa
BoT, Prof. Benno Ndulu, alisema malipo ya fedha kutoka akaunti ya Escrow, Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia Wizara ya Nishati na Madini na IPTL zilisaini makubaliano ya kutoa
fedha zilizomo katika akaunti hiyo ili zilipwe kwa IPTL.
Alisema makubaliano hayo yalijulikana kama
“Agreement for Delivery of Funds to Independent Power Tanzania Limited” ambapo
yaliambatana na muhtasari wa kikao cha pamoja cha uhakiki wa malipo ya tozo
kati ya IPTL na TANESCO, pamoja PS –MEM ikiwasilisha makubaliano hayo na
kuiomba BoT iruhusu malipo hayo kwenda IPTL kama
uhakiki ulivyobainisha.
“Kwa mujibu wa kifungu 7.7 cha makubaliano ya
ufunguzi wa akaunti (Escrow Agreement) fedha zilizomo kwenye akaunti hiyo
zingeendelea kuwepo na kuwa katika mamlaka ya Escrow na kwamba fedha hizo
zingetolewa tu kama kuna hukumu ya mahakama
inayoamuru kutolewa kwake au pande mbili za makubaliano,”alisema.
Aidha alisema Septemba 5 mwaka 2013,mahakama kuu
ya Tanzania ilitoa uamuzi uliogusa umiliki wa fedha zilizopo katika akaunti
hiyo,iliyokuwa chini ya udhibiti wa BoT,kutokana na uamuzi huo uliotokana na maombi yaliyofanywa na
mmoja wa wanahisa wa IPTL- VIP (Engineering and Market Limited) ambaye aliomba
mahakama iridhie kufutwa kwa shauri ambalo VIP walilifungulia mahakamani (Misc.Civil
Application No.49/2002 na Misc.Civil Application No.254/2003.
Alibainisha kuwa maombi hayo yalitokana na
makubaliano ya mauzo ya hisa za VIP katika IPTL kwenda katika kampuni ya Pan
Afrika Power Solutions (T) Limited PAP.
Alisema katika uamuzi huo,mahakama pamoja na mambo
mengine iliridhia kufutwa kwa mashauri na kuelekeza kwamba mali zote za
IPTL,ikiwemo kiwanda cha kufua umeme zikabidhiwe kwa mmliki mpya wa IPTL ambaye
ni PAP.
Hata hivyo alisema fedha za ‘capacity charge’ ziligawanyika
katika makundi mawili moja fedha za kitanzania wakati kiasi kingine ni dola za Marekani.
Alianisha makundi hayo ya fedha yalikuwa
yamewekezwa katika uwekezaji wa ndani na wa nje, kwa kuzingatia kifungu 3.4 cha
escrow agreement, ambapo hadi kufikia Novemba 25 mwaka 2013,salio katika dola
za Marekani,pamoja na faida ilikuwa ni dola 22,198,544.60,huku salio katika
fedha za kitanzania zilikuwa ni shilingi 161,389,686,585.34 ikijumuishwa na
faida katika uwekezaji shilingi 5,297,550,682.04.
Alisema Julai 5 2006 serikali kupitia Wizara ya
Nishati na Madini na IPTL pamoja na BoT,
waliingia makubaliano ya kufunga akaunti maalum (escrow).
No comments:
Post a Comment